YANGA WAKUMBANA NA MVUA KUTENGENEZA UWANJA WAO - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 11, 2017

YANGA WAKUMBANA NA MVUA KUTENGENEZA UWANJA WAO



Club ya yanga ambayo kwa hivi sasa ipo katika mchakato wa kukarabati uwanja wao wa kaunda uliopo makao makuu ya
timu hiyo jangwani, imejikuta ikipata changamoto kubwa katika kuhakikisha kuwa inaukarabati uwanja huo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kikwazo cha mvua nyingi pamoja na vifusi vikubwa ambavyo kuviondoa ni gharama kubwa.
Boniface mkwasa alipohojiwa alikuwa na haya ya kusema.

“Kuna changamoto nyingi ambazo tunakumbana nazo katika maendeleo ya ujenzi wa uwanja, vifusi vimekuwa havipatikani, tumekuwa tukisaka kila mahali na pale tunapovipata inakuwa ni gharama kubwa kuvifikisha hapa klabuni.
“Mvua pia imekuwa kikwazo kikubwa kufanikisha zoezi letu hilo la upatikanaji wa vifusi, lengo letu ni kuhakikisha tunafanikiwa kumaliza ndani ya wakati lakini changamoto hizo zinatukwamisha, tutaendelea kupambana nazo.

“Kuhusu gharama ambazo tutazitumia kutengeneza uwanja hadi sasa bado hatujazifahamu, kwani mchakato wa awali uliopo ni kujaza vifusi kisha hapo baadaye ndiyo tutajua tutatengeneza uwanja wa aina gani na kufahamu gharama halisi, tuna mainjinia wengi pamoja na wadau mbalimbali ambao wataweza kufanya mchakato huo wa mchanganuo wa ujenzi wa uwanja kwa ujumla,” alisema Mkwasa.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();