MWANAUME AFUNGA NDOA NA WAKE WATATU KWA MKUPUO - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 20, 2017

MWANAUME AFUNGA NDOA NA WAKE WATATU KWA MKUPUO



Mwanaume mmoja huko nchini uganda, ameweka historia ya funga mwaka mara baada ya kupiga harusi moja matata iliyohusisha wanawake watatu ambao alifungishwa nao ndoa. Mwanaume huyo ni muuzaji wa vyakula

Mohammed Ssemada anayetoka katika kabila la Wagisu nchini Uganda amefunga ndoa na wanawake wa tatu, Salmat Naluwugge, mwenye umri wa miaka 48 ambaye ana watoto wa 5, Mastulah Nawanje 24, pamoja na Jameo Nakayiza 27.
Harusi hiyo ilifanyika katika mji Wakiso huku umati wa watu walioshuhudia wakibaki mdomo wazi.
Kilichowashangaza wengi ni kwamba mke wa kwanza Naliwugge ni mama wa watoto 5 na amekuwa katika ndoa na Ssemada kwa muda wa miaka 20.
Ingawa Ssemada amethibitisha kwamba yeye kipato chake ni cha chini ila alionyesha furaha kubwa kwa wake hao waliomkubali licha ya kipato chake hicho duni.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, Naluwugge alimshukuru Mungu kwa kuifanikisha  harusi hiyo, ”Namshukuru mume wetu kwa kutuoa soote kwa siku 1. Kwangu, ni ishara tosha kwamba hatambagua yeyote”.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();