STORY:MARI YA KAFARA
SEHEMU YA-3
MWANDISHI#Amany Zabranco.
POSTED@Mainfo93.com
Sehemu iliyopita iliishia pale shabibi alipokuwa akiambiwa na yule binti asogee, lakini shabibi akawa anagoma kusogea, sasa twende nayo.
Yule dada akamsogelea shabibi kisha akamuambia kwenye sikio,
"Nakutaka naomba tuondoke wote hadi unapoenda".
Shabibi kuambiwa vile akawa anawaza ni jinsi gani ataondoka naye hali ya kuwa yeye anaenda kwenye hicho kijiji ambacho hata siku moja hajawahi kufika huko.
Shabibi ikabidi amkubalie yule binti ili apate campany ya kwenda kwa mganga, safari ikazidi kwenda, ikiwa ni majira ya jioni tayari gari likawa limekaribia kufika.
Hatimaye kituo ambacho hilo gari linaishia wakapafikia, shabibi akashuka na yule binti kisha wakasogea pembeni kidogo, shabibi ikabidi amueleze yule binti mahali anapoenda, akamuambia anaenda kwa mganga kuna shida fulani anahitaji kuitatua.
Yule dada kwa kuwa alipata miujiza akawa kila kitu anachoambiwa na shabibi yeye anakubali tu, shabibi ikabidi amuulize jina lake yule binti.
Shabibi akauliza, "samahani dada jina lako ni nani?".
binti akajibu "naitwa meresia na wewe unaitwa nani?."
Shabibi akajibu "Naitwa shabibi".
Meresia akasema, naomba tuanze kuelekea huko kwa kuwa muda unaenda.
Shabibi akamuuliza meresia "Unapafahamu huko".
Meresia akajibu"ndiyo napafahamu vizuri ni kuvuka mto, na mitumbwi huwa ipo hata usiku".
Wakachukua usafiri wa baiskeli kwa kuwa eneo hili ndizo hutumika kama daladala,
wakaanza kuelekea kwenye huo mto kwa ajiri ya kuvuka ili kuingia kwenye hicho kijiji.
Wakatumia dakika kadhaaa, kisha wakafika ng'ambo ya huo mto, yule aliyekuwa kampakiza shabibi akasema "tumekaribia, ni pale mbele unapopaona.
Wakafika na kushuka kwenye baiskeli, wakamlipa yule daladala kisha wakaanza kusogea hadi kando kando ya ule mto, shabibi akawa anashangaa kuona hali tulivu huku kukiwa hakuna kelele zozote zile kwenye ule mto.
Shabibi akasogea akachota kidogo maji ya ule mto akajipaka utosini, mara hali ya ujasiri ikamjaa, wakachukua mtumbwi mmoja kisha wakaanza kukatiza ndani ya maji kuelekea ng'ambo ambapo kipo hicho kijiji.
Mtumbi ulipofika katikati ya maji mara ghafra kichwa cha shabibi kikawa kizito ile ndoto aliyoiota akawa anahisi inajirudia rudia akilini mwake, akawa anawaza mambo ya ajabu, yule binti ikabidi amshike shabibi akawa anamuuliza kama ana tatizo lolote lakini shabibi akawa anasema hapana kitu chochote, yule aliyekuwa akiendesha ule mtumbi akawaambia kina shabibi, jamani kuweni makini sana huu mto una maajabu na sahivi muda umeenda sana,
Baada tu ya kusema yale maneno mara kwa mbele wakaona samaki mtu ameibuka toka ndani ya maji, aka..............(ITAENDELEA @MAINFO93.COM. #Amany Zabranco).