SIMULIZI: #MALI YA KAFARA.
SEHEMU YA-1
MWANDISHI:Amany Zabranco.
sehemu inayopostiwa ni mainfo93.com.
Karibu sana mainfo93.com.
Simulizi iitwayo MALI YA KAFARA ni simulizi ya kusisimua inayomhusu kijana mmoja ambaye kutokana na hali duni ya maisha,anaamua kusafiri hadi kwenda kwenye kijiji flani kwa ajiri ya kwenda kutafuta mganga wa kumsaidia nyota ya fedhwa. Simulizi hii ndo kwanza bado mbichi kabisaaaa, so kaaa mkao wa kula kuifatilia. Itakuwa inapatikana mainfo93.com. So jitahidi kuingia google na kusachi mainfo93.
Simulizi inaanza kwa kijana mmoja aitwaye Shabibi ambaye alizaliwa katika mtaa wa Mabanda saba unaopatikana katika moja ya miji mikubwa. Mtaa huo ulikuwa ni maarufu kwa kuwa watu wake ni wa hali ya chini sana kiuchumi,hata majengo ya mtaa huo mengi ni nyumba duni kana kwamba ukiziona utazani zilijengwa miaka ya elfu moja mia nane na kenda.
Kutokana na hali hiyo,kijana shabibi siku moja akawa amekaa nje ya nyumba yao ya tope huku mabati yakiwa yamepauka utazani unga wa dona, shabibi akawa anaangalia nyumba yao huku mawazo kichwani yakimuijia,akawa anaongea peke yake kimoyomoyo.
"Hivi haya maisha nilipewa? au niliokota,? vyuma vimekaza kama super grue, lazima nitoke,lazima lazima,lazima!!".
Baada ya shabibi kuwa anawaza vile mara akatoka nje dada yake akaita,
"we shabibi?? shabibi!?.
Shabibi alikuwa mbali sana kimawazo akawa hata hastuki,dada yake akamsogelea akamgusa mgongoni, shabibi akaruka kwa mshtuko, kisha dada yake akaanza kucheka.
"Hahaaaaaaa!!! hahhhhaaaaa!!!,kumbe nawewe huaga muoga hivyo?".
Shabibi akawa hajibu kitu huku akimuangalia dada yake machoni kwa jicho kali kama jambazi aliyeona pesa.
Dada yake akamuuliza, "Shabibi vipi mbona umemaindi kihivyo? unawaza nini?."
Shabibi akajibu "Unareta ujinga sindio?".
Dada yake akamjibu kwa sauti ya upole.
"Basi nisamehe bure!".
Shabibi hakujibu kitu akawa bado anamuangalia dada yake kwa hasira. Dada yake akamuuliza tena.
"We shabibi leo una nini? au umetoswa na demu wako mihasira unaileta kwangu?".
Shabibi akakasirika akamsogelea dada yake akampiga kofi moja matata, dada akapiga kelele.
"Mamaaaaaa nakufaaaaaaaaa maaamaaaaaa...!!".
Mama yake akaja huku anahema juujuuu akauliza "mwanangu kuna nini?."
Dada akajibu "mama shabibi kanipiga".
Mama akakasirika akasema "hivi weweeee!! hicho kijifua chako ndo kinakupa kiburi sio?, kama unanguvu si ukabebe mizigo upate hela ya kunyoa hiyo minywele yako".
Shabibi akawa kimya huku kifuani akionekana amefura mithili ya chatu mwenye hasira, kifua kikawa kinatuna kwa hasira, shabibi akasogea ukutani akaanza kupiga ukuta kwa nguvu na hasira nyingi.
Mama akamshika mkono dada wa shabibi kisha akasema, "mwanangu twende ndani tusije tukavyunjwa bure,".
Wakaingia ndani,nje akawa amebaki shabibi peke yake, taratibu hasira zikaanza kushuka, akakaa chini huku rundo la mawazo likiwa limemzonga.
Baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa, mara likaja wazo kichwani, akakumbuka aliwahi kusimuliwa na rafiki yake kuwa alienda kwa mganga kijiji fulani akapewa dawa ya mali, hadi sasa rafiki yake huyo anamiliki maduka makubwa 7, nyumba tatu nzuri pamoja na gari za daladala mbili na moja ya kutembelea.
Hapo ndipo roho ya kijasiri mithiri ya raisi wa korea kaskazini ikamjaa shabibi, wazo likawa moja, ni kwenda kwa huyo mganga ambaye anapatikana kwenye kijiji kilichopo pembezoni mwa mto magudura, mto ambao ni wa ajabu, watu maarufu,wafanya biashara na matajiri wakubwa wote huenda kutoa kafara kwenye mto 'MAGUDURA' kila mwisho wa mwaka ili mipango yao inyooke kwa mwaka unaofuata.
Sasa shabibi akanyanyuka taratibu akaingia kwenye chumba chake akaanza kufungasha nguo ili asubuhi aondoke kwenda huko, ilipofika usiku, dada yake akamletea chakula chumbani kwake. Wakawa wamesameheana wakawa wanacheka pamoja.
Muda wa kulala ukafika, shabibi akachukua lile begi lake akaliweka pembeni, kisha akachukua karatasi iliyokuwa imeandikwa maneno ya kishujaaa "USIKUBALI KUFA BILA YA KUISHI VIZURI".
Usiku ulipofika shabibi akiwa usingizini akaota..........(Je itakuwaje?. Usikose kufuatilia hii kitu hapa mainfo93.com. Like fb page @mainfo93. join fb group @ MAGAZETI YA LEO. #Composed with love @Amany Zabranco. follow me