ASIMULIA ALIVYOKATWA MIKONO NA NGURUWE - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 20, 2017

ASIMULIA ALIVYOKATWA MIKONO NA NGURUWE



MTOTO Farida Silvanus (15), mkazi wa Perege Wiliya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,amewashangaza watu kutokana na vitu anavyofanya huku akiwa ana mikono yote miwili.

Akizungumza na Global TV, Farida amesema kuwa alipata ulemavu huo wa kukatika mikono baada ya kung’atwa na Nguruwe akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu wakati mama yake alipokuwa ameenda kisimani kuchota maji.
Amesema, kuwa mama yake huyo alimuacha kitandani ndipo Nguruwe, aliposukuma mlango kwa kishindo kisha kumvuta kitandani na kumsokomeza uvunguni na kuanza kutafuna mikono yake yote miwili pamoja na kidevu.
Akisimulia zaidi mkasa huo, Farida amesema, baada ya mama yake kuona hivyo alipiga kelele na majirani walikuja na kuamua kunipelekea katika hospitali ya mkoa wa Iringa,ambapo alipatiwa matibabu hapo..
Japokuwa ana changamoto ya kukosa mikono yote mtoto Farida, anaweza kufanya kila kitu anachofanya mtu ambaye ana mikono yote miwili huku akitamani kupata mikono bandia.


'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();