AJICHARANGA VIWEMBE KWA KUACHISHWA KAZI YA KUOSHA MAGARI-KAHAMA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 14, 2017

AJICHARANGA VIWEMBE KWA KUACHISHWA KAZI YA KUOSHA MAGARI-KAHAMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Adam (18) a





Amejichana chana na wembe sehemu za kichwani hali iliyosababisha atokwe
damu nyingi kwa kile kinachodaiwa kuwa ameachishwa kazi ya kuosha mabasi ya Kampuni ya Rungwe mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea leo Alhamis Disemba 14,2017 majira ya saa tatu asubuhi, baada ya kijana huyo kwenda kwa mwajiri wake kudai arejeshwe kazini lakini alikataliwa na kudaiwa kuanza kufanya fujo na kisha kufikishwa kituo cha polisi Kahama.
Mmoja wa Mashuhuda amezungumzia tukio hilo na kudai kuwa imetokea baada ya kijana huyo kuwa amelewa sana.
Naye wakala wa mabasi ya Rungwe John Lucas ambapo kijana huyo alikuwa anafanya kazi amesema kijana huyo aliachishwa kazi ya kuosha mabasi ya kampuni hiyo zaidi ya wiki mbili na kwamba leo alifikia hapo saa 12 asubihi kuomba arejeshwe kazini huku akitumia nguvu kudai maombi hayo.
Hata hivyo wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamempeleka katika hospitali ya mji wa Kahama kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();