ERIC BAILLY WA MAN U. NJE KWA MIEZI MITATU - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 16, 2017

ERIC BAILLY WA MAN U. NJE KWA MIEZI MITATU


Beki wa Manchester United Eric Bailly
atafanyiwa upasuajiwa kifundo cha mguu na kukaa nje miezi mitatu
Bosi wa United Jose Mourinho alisema katikati ya juma kuwa beki huyo wa kati atapigwa kisu kurekebisha tatizolae, na amethibitisha Ijumaa kuwa hofu yake imedhihiri.
"Anakwenda kufanyiwa upasuaji, uamuzi umefanyika," Mourinho alisema. "Sisemi kwamba yupo nje kwa muda wote wa msimu, lakini kwa miezi mitatu ijayo."
Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Bailly amekosa mechi nane mfululizo, na mechi ya karibuni aliyocheza ni ile waliyofungwa 1-0 na Chelsea November 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipata majeraha kwenye majukumu ya kimataifa lakini Mourinho alisema mapema juma hili kuwa anaridhishwa na wanaoweza kuziba pengo lake.
Alisema: "Nimemchezesha [Chris] Smalling na [Phil] Jones na tunaye [Victor] Lindelof na [Daley] Blind kwenye benchi. Marcos Rojo alipata majeraha [dhidi ya Manchester City] lakini tatizo si kubwa.
"Katika msimu wote, tumekuwa na tatizo la mabeki wa kati, lakini kwa sababu namba ni nne au tano, mara zote tunaweza kutumia wachezaji tulio nao.
"Chris Smalling anacheza vizuri sana kwa mechi saba au nane mfululizo, kwa hiyo tuko vizuri."
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();