YANGA WAFUNGUKA SABABU ZA KUTOSAJIRI SANA DIRISHA DOGO - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 21, 2017

YANGA WAFUNGUKA SABABU ZA KUTOSAJIRI SANA DIRISHA DOGO



Club ya yanga imetolea ufafanuzi jambo la wao kutofanya usajiri mkubwa katika dirisha dogo kwa kile walichodai kuwa hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.


Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wasingefanya usajili kwa kuwa kulikuwa na wachezaji wengi majeruhi ambao walikuwa wanarejea kundini.
"Ukiangalia wachezaji wengi ndiyo walikuwa wanarejea kundini wakitoka kujiuguza. Sasa hauwezi kufanya usajili mkubwa badala yake kuhakikisha wanapona.
"Baada ya hapo, tutaanza kuangalia perfomance (utendaji), mbele huko tutajua kama tunapaswa kuongeza wachezaji au la," alisema.
Yanga ilisajili wachezaji wawili tu akiwemo kinda Yohana Mkomola na usajili wake haukuwa na zaidi ya hapo.
Wachezaji wengi wakongwe wa Yanga walikuwa majeruhi kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi lakini Yanga wana furaha kwa kuwa wote wameanza mazoezi.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();