HAJI MWINYI AZIDI KUJAA KIBURI, AWAPA YANGA MASHARTI, WAKIZINGUA ANASEPA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 20, 2017

HAJI MWINYI AZIDI KUJAA KIBURI, AWAPA YANGA MASHARTI, WAKIZINGUA ANASEPA



Beki wa kushoto wa yanga,Haji Mwinyi ambaye kwa sasa yupo hot kwenye kutakiwa na vilabu huko kenya. Amewapa masharti yanga kuwa wampe fursa ya kuanza kikosini sio kuwekwa benchi na Gadiel Michael lasivyo ataamua kuandika barua ya kuachwa.
Kwa sasa AfC Leopard ya kenya inamuhitaji Haji mwinyi kwa udi na uvumba baada ya kukubali makeke yake akiwa na zanzibar heroes.


“Nashukuru Mungu kwa kuweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Chalenji, ukweli siyo kwamba nimeisha isipokuwa tu kuna mambo madogomadogo ndiyo yalikuwa yanatatiza kwa upande wangu lakini kila mmoja ameona nilichokifanya Kenya.

“Najua Gadiel Michael ni mchezaji mzuri amenipa changamoto kubwa na naamini nafasi yangu ya kucheza ipo wazi katika kipindi hiki labda yatokee mambo mengine ila kocha akinipa nafasi kila mmoja atafurahia kazi yangu hasa mashabiki wetu wa Yanga na kama itashindikana basi nitaomba niachwe ili niweze kwenda sehemu itakayopata nafasi ya kucheza," alisema Mwinyi.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();