STORY:MALI YA KAFARA:SEHEMU YA-4 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 21, 2017

STORY:MALI YA KAFARA:SEHEMU YA-4



STORY:MALI YA KAFARA
SEHEMU YA:4
MWANDISHI:Amany Zabranco
POSTED @MAINFO93.COM
Sehemu iliyopita iliishia pale shabibi na meresia walipokuwa ndani ya ule mto, mara ghafra akatokea samaki mtu kisha akawa anausumbua ule mtumbwi. sasa songa nayo.


Yule samaki mtu akaushika ule mtumbwi kisha akaubinua na kuubwaga ndani ya maji, shabibi na meresia pamoja na yule muendeshaji wa mtubwi, wote wakawa wanatapatapa kutafuta namna ya kuogelea ili wajiokoe, sauti za wanawake zikawa zinasikika ndani ya maji, wakiwa wanapiga mayowe huku wakiimba nyimbo za kutisha.

Shabibi akawa anajitahidi kumsogelea meresia, lakini meresia akawa anaelemewa na maji ya ule mto,akawa anapiga kelele ili shabibi asogee kumsaidia, shabibi akazidi kujikaza kwa nguvu zake zote hadi akasogea karibu ya meresia, yule muendeshaji wa mtumbwi kwa kuwa alikuwa mzoefu wa jinsi ya kupiga mbizi akawasogelea kina shabibi kisha akawaambia wamshike ili awasaidie, wakamshika akaanza kupiga mbizi mithiri ya mashindano ya olympic.

Hatimaye wakafanikiwa kufika ukingoni mwa ule mto huku wote wakiwa wamechoka vya kutosha, wakawa wamelowa maji kila mmoja akawa anajaribu kujikamua nguo zake.

Kwa kuwa usiku ulikua umeshaingia isitoshe kufika kwenye hicho kijiji ilikuwa bado ni umbari mrefu, yule mwendesha mtumbwi akawaambia kina shabibi kuwa hawawezi kupata mtumbwi mwingine hadi asubuhi kwahiyo inabidi waanze kutembea. Ilikuwa ni ndani ya pori nene lililoshamiri miti ya kijani kibichi.

Wakaanza kutembea ndani ya pori huku yule muendeshaji akiwa anawaongoza wasije kupotea, wakazidi kusonga ndani ya lile pori wakatembea kwa muda mrefu,sasa usiku ukazidi kupanda.

Yule muendesha mtumbi akawaambia ni bora wapumzike ili asubuhi watafute msaada, kweli wote kwa kuwa walikua wamechoka vya kutosha ikabidi wakubaliane na wazo  lake. Wakasogea hadi sehemu fulani ndani ya pori,kulikua na mti mkubwa sana  chini yake kuna kichaka kikubwa kimejitengeneza kama hema flani,kisha wakaanza kupasafisha pale chini wakakaa.

Yule muendesha mtumbwi akasimama akaanza kutafuta kuni, akakusanya rundo la kuni kisha akaliweka pembeni, akaichambua akatengeneza vizuri kwa ajiri ya kuwasha moto.
Kwa kuwa hakua na kiberiti ikabidi achukue kinyesi cha mnyama kisha akaanza kukipikicha utazani mtu wa kale, moto ukawaka na kukolea vizuri wote wakauzunguka moto kuota,huku wakipiga story za hapa na pale.

Ghafra sungura akawa anajipitisha kwenye kile kichaka, shabibi akamuona akasimama kimyakimya akaanza kunyata taratibu akazunguka nyuma ya kichaka akamrukia yule sungura akamkamatilia chini.
Meresia akafurahi sana akasema
"inaonekana wewe ulikuwa muwindaji mzoefu sana.
Shabibi akajibu
"hamna ni uzoefu wa kudaka mpira ndo maana sijamkosa".

Yule mwendesha mtumbwi akamshika sungura,kwa kuwa mfukoni mwake alikua na kisu kidogo ikabidi wamchinje wakaanza kumchoma.

Kwa kuwa kila mmoja alikua na njaa mate yakawa yanakimbizana mdomoni kwa kuwa kila mmoja alikua anahamu kwa jinsi ile nyama inavyoiva huku ikitoa mafuta mafuta.
Ghafra ikatokea..............(ITAENDELEA @MAINFO93.COM. CRafted in love with Amany zabranco. Kupata story zote za mr.Zabranco contact #mainfo93@gmail.com list _MJUKUU WA MSUKULE_SIRI YA MAITI_ROHO YA KUZIMU_KISIWA CHA MAJINI_FUMANIZI. )

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();