HAJI MWINYI APATA MASHAVU, HII HAPA TIMU INAYOMTAKA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 19, 2017

HAJI MWINYI APATA MASHAVU, HII HAPA TIMU INAYOMTAKA



Baada ya zanzibar heroes kuonyesha umakini mkubwa katika michuano ya huko kenya, sasa wachezaji wengi wa timu hiyo wameanza kumezewa mate na vilabu mbalimbali.
Kwa upande wa beki wa yanga, haji mwinyi, licha ya kusota mda mrefu kwa kusugua bench ndani ya yanga, sasa AFC LEOPARD ya kenya imesema inamhitaji haji mwinyi.


"Siwezi kukata ofa kama hiyo lakini mimi bado ni mchezaji wa Yanga kwasababu ninamkataba nao ispokuwa kama wanaweza kunisubiri nimalize mkataba wangu sawa au wazungumze na waajiri wangu kama wataelewana nipo tayari kujiunga nao," amesema Mwinyi.
Beki huyo ambaye hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Yanga ni miongoni mwa wachezaji wa Zanzibar Heroes, aliyengara kwenye michuano hiyo na kutengeneza pasi ya mabao mawili katika mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji Kenya.
Mbali na Mwinyi mchezaji mwingine ambaye ameonyesha kuivutia klabu hiyo ya Leopard ni kiungo Abdulaziz Makame ambaye naye anahitajika nchini Kenya kujiunga na timu hiyo.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();