STORY:MALI YA KAFARA :SEHEMU YA-2 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 18, 2017

STORY:MALI YA KAFARA :SEHEMU YA-2

       

         STORY:MALI YA KAFARA
         SEHEMU YA-2
          MWANDISHI-#Amany Zabranco.
           posted @mainfo93.com
Sehemu ya kwanza tuliishia pale shabibi alipolala usiku akijiandaa asubuhi kwenda kwenye kile kijiji alipo yule mganga.
Sasa endelea kutiririka nayo.

Usiku ukafika huku shabibi akiwa amelala mara ndoto ya ajabu ikamtokea,akawa anaota yupo ndani ya mtumbwi akikatiza mto uliokuwa unaelekea kijiji cha
kando kando ya mto, lakini ule mtumbwi akaona watu wawili wakiwa wamevaa mavazi meupe huku wakiwa hawaongei kitu chochote. Shabibi akawa anawaogopa wale watu akawauliza.
  "Tunaenda wapi jamani??". Wale watu hawakugeuka nyuma wakaendelea kusonga mbele bila ya
kumuongelesha shabibi, wakafika hadi katikati ya ule mto, mara ghafra kwa mbele akatokea samaki mtu wa kike akasimama juu ya maji, shabibi akawa anamshangaa.
 

Lakini cha ajabu wale watu hata hawakuwa wakihofia chochote wakazidi kumsogelea yule samaki mtu huku wakiwa ndani ya mtumbwi.
Walipomkaribia zaidi yule samaki mtu wakataka kumpamia, samaki mtu akaushika mtumbwi akataka kuubwaga majini, ghafra shabibi akastuka toka usingizini.

Shabibi akawa anahema juujuu kwa woga, akawa anaitafakari ile ndoto lakini akawa hapati jibu, akawa anawaza ahirishe kwenda ila moyo ukawa unakataa akawa na roho ya kijasiri akajitamkia mwenyewe.

"Kufa au kupona,lazima nifanikishe huu mpango".
Sasa shabibi akaamua kutolala ili asipate ndoto, akachukua kitabu cha hadithi kilichoandikwa "KISIWA CHA MAJINI", Kisha akaanza kukisoma usiku ukapita, asubuhi na mapema jogoo wakawa tayari wanatekeleza jukumu lao la kuamsha watu.

Shabibi akachukua begi lake akavaa mgongoni kisha akatoka kimya kimya huku kukiwa hakuna hata mmoja anayefahamu kama shabibi anaondoka nyumbani. Shabibi akatoweka kisha akapanda gari liendalo eneo la karibu na kile kijiji.

Shabibi akaianza safari huku ndani ya gari akiwa amejawa na mawazo mengi kuhusu ile ndoto, alipoona mawazo yanazidi akafungua begi lake kisha akakitoa kile kitabu cha "KISIWA CHA MAJINI".Akaanza kukisoma mule ndani ya gari, abiria mmoja wa kike aliyekuwa amekaa pembeni ya shabibi, akamuuliza

"Samahani mkaka naomba nikione hicho kitabu inaonekana kina story nzuri"!.
Shabibi akamuambia yule dada
   "Lakini kina tisha sana dada yangu".
Yule dada akajibu hapana nipe tu nikione nimekipenda!".

   Shabibi akampa kile kitabu yule dada, lakini alipompa tu, yule dada alipokishika, akahisi kichwa kimekuwa kizito, akaanza kumpenda shabibi, akaanza kupenda aondoke naye.

  Yule dada akakifungua akaanza kukisoma, akasoma kidogo tu, lakini miujiza ikamjaa akampenda shabibi kupita kiasi akamuambia.

"Kaka.sogea".
Shabibi akastuka akauliza kuna nini tena?.
Yule dada akasema tena "please we sogea tu!
Shabibi kwa woga akawa anagoma ila yule dada aka.............(ITAENDELEA . INGIA MAINFO93.COM.). crafted In love with #AMany Zabranco.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();