ASILIMIA 49 ZA MO NA 50 ZA WANACHAMA ZAWA PASUA KICHWA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 14, 2017

ASILIMIA 49 ZA MO NA 50 ZA WANACHAMA ZAWA PASUA KICHWA



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema
uwekezaji unapaswa kuwa asilimia 49 kwa muwekezaji Mohammed Dewji na 51 inabaki kwa wanachama.
Mwakyembe aliyasema hayo wakati alipojitokeza katika udhamini wa kampuni ya Biko kwa timu ya Stand United.
Kauli yake ilikuwa ni kufafanua baada ya wanachama wa Simba kupitisha uwekezaji wa asilimia 50 kwa 50.
Baada ya hapo, kumekuwa na mjadala mkubwa hasa mitandaoni, wengine wakiona sawa na wengine wakiona si sawa.
Mfumo wa 49 kwa 51 zaidi unatumika katika Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Awali, Dewji aliwahi kusema alikuwa akiweka Sh bilioni 20 ili kuwekeza kwa asilimia 51.
Baadaye ilionekana haiwezekani na mwisho makubaliano yakawa ni asilimia 50 kwa 50 lakini kauli hiyo ya serikali imeamsha mjadala mpya.
Wanaounga mkono wanaona ni sahihi wengi kuwa na nguvu jambo ambalo serikali inaamini lakini wengine wanaona anayetoa fedha pia ana haki ya kuwa na nguvu zaidi.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();