HANS PLUIJM APEWA MTIHANI WA KWANZA SINGIDA UNITED - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 18, 2017

HANS PLUIJM APEWA MTIHANI WA KWANZA SINGIDA UNITED


Singida united kwa mara ya kwanza imepewa fursa ya kushiriki kombe la mapinduzi ambalo litaanza kutimua vumbi tarehe 29 december. Uongozi umemuambia pluijm ahakikishe anachukua
mapinduzi cup.

Singida ambayo imepanda daraja msimu huu itashiriki Mapinduzi kwa mara ya kwanza ikiwa kundi moja na Yanga, Mlandege, Taifa Jangombe, Zimamoto na JKU ambazo zipo Kundi B huku Kundi A zikiwa timu za URA, Jamhuri, Mwenge, Simba na Azam FC.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amesema kuwa, lengo lao kubwa ni kuona wanafanikiwa kutwaa kombe hilo, japokuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika michuano hiyo, hivyo wanahitaji kufanikiwa kufanya vyema.
“Tunashukuru kuitwa kushiriki michuano ya Mapinduzi na ni jambo la kheri sana, tutakwenda kwenye michuano kwa ajili ya kupambana na si kushiriki japokuwa itakuwa ni mara yetu ya kwanza.
“Tunahitaji kombe hili pia liweze kutua Singida kwa mara ya kwanza, tunaitumia michuano hii kama maandalizi kwetu kwa ajili ya ligi kuu na hatuendi kwa ajili ya kujifurahisha.
“Kikosi chetu kipo vizuri, tunaamini uwezo wa kutwaa kombe hilo upo chini ya kocha wetu Hans Pluijm,” alisema Sanga
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();