UDHAMINI WAIDATISHA MBAO,WASEMA YANGA HACHOMOKI LEO - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 31, 2017

UDHAMINI WAIDATISHA MBAO,WASEMA YANGA HACHOMOKI LEO



Suala la Mbao FC kupata mdhamini mpya kupitia bidhaa za maziwa ya Cowbell, inaonekana kuwachanganya na kutotaka kushindwa mechi ya leo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

Mbao FC watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo na tayari wako kambini kukiwa na hamasa kubwa kutaka kushinda mechi hiyo.

Taarifa zinaelezwa, wachezaji wa Mbao FC wameahidiwa motisha kama wataishinda Yanga na inaelezwa hamasa imeongezeka kutokana na suala la mdhamini.

"Kweli wachezaji wamesisitizwa sana kushinda leo kwa mambo matatu. Kwanza wakishinda watakuwa wameongeza hali ya kujiamini, pili watakuwa wameongeza pointi tatu ambazo ni muhimu sana.

"Lakini hili la tatu limezungumziwa sana, ni suala la mdhamini kwamba atashawishika zaidi kuona kuwa hajakosea kuidhamini Mbao FC kwa kuwa wanajua naye atatupa jicho la karibu katika mechi hiyo," kilieleza chanzo.

Mbao FC hata kabla ya kupata mdhamini imekuwa ikiisumbua Yanga kwa kiasi kikubwa. Iliwahi kuing'oa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga hapohapo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();