AISHI MANULA AWA MCHEZAJI BORA SIMBA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

December 10, 2017

AISHI MANULA AWA MCHEZAJI BORA SIMBA



Kipa namba moja wa klabu ya Simba na Taifa Stars Aishi Manula, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo katika
mwezi Novemba, baada ya kutoa mcnago mkubwa kwa timu yake hadi kufanikiwa kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Msemaji wa Simba Hajji Manara, ameiambia Goal, kuwa Manula ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Mohamed Hussein 'Tshabalala' na James, ambao nao walifanya kazi kubwa ya kuipigania timu hiyo katika mechi za ligi mwezi huo.
"Tunampongeza Manula, kwa kutwaa tuzo hiyo kutokana na mchango wake naamini itamuongezea ari ya kujituma na kuipigania Simba, izidi kufanya vizuri katika michuano yote ambayo tunashiriki msimu huu," amesema Manara.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Manula kutwaa tuzo hiyo tangu alipojiunga na Simba, akitokea Azam FC, timu ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa tangu alipoanza kucheza soka la ushindani aitokea Morogoro.
Simba imekuwa na utaratibu maalumu wa kuchagua mchezaji bora na kutoa zawadi ya laki tano 500,000, ili kutoa hamasa na changamoto kwa wachezaji wake kuzidi kujituma na kupata mafanikio katika kufikia malengo yao.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();