Shirika la umoja wa mataifa wfp na unseco yote kwa pamoja
yamegawa tablets kwa wanafunzi wa shule ya msingi kwenye kijiji kimoja huko tanga ili watumia katika masomo yao. Aidha wanafunzi wapatao 2400 watanufaika na mpango huo kwenye kijiji hicho.
Tablet hizo ziligawiwa kama sehemu ya mradi wa majaribio wa miezi 15 chini ya Global Learning XPRIZE ambao ni mradi wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 15.
Mradi huu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wabunifu kubuni na kuandaa zana-wazi za kiteknolojia ili kuwawezesha watoto walio na fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).