“Tayari klabu zote za Simba na Yanga zimeshawasilisha majina
ya usajili wa wachezaji wao wote Caf kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
“Ratiba ya makundi inatarajiwa kupangwa leo’ nchini Misri hivyo tutapata fursa ya kutambua Simba itacheza na nani na Yanga itacheza na nani kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michuano hiyo.
“Kawaida usajili wa kimataifa katika michuano Caf lazima wataacha nafasi kwa ajili ya kuongeza wachezaji wengine hapo baadaye, kwa upande wa Simba na Yanga wamepeleka majina ya wachezaji wao wote waliowasajili lakini hawakufikia idadi ya wachezaji 30 ambayo ndiyo ya mwisho,” alisema Lucas.
Simba na Yanga zimekuwa zikifanya vizuri kila zinapokutana na timu nyingine, lakini zinapokutana na timu kutoka kwenye nchi za Kiarabu mambo huwa magumu, hivyo hawataki kabisa kukutana na hali hiyo.
Toimu vigogo ambazo Yanga hawataki kukutana nazo na zipo kwenye Klabu Bingwa Afrika ni Al Ahily, Esperance, Etoile du Sahel, TP Mazembe, Waydad Casablanca na ES Setif.
Simba wenyewe watakuwa wanakwepa kukutana na Zamalek, Enyimba, Raja Casablanca, Supersport United na USM Algier.