Karibu mainfo nainte three kwa mainfo yote ya kimichezo bongo na mbele
"Nikweli tumeachana na
Mwanjali lakini ni makubaliano maalumu, hiyo inatokana na hali ya afya yake kuwa majeruhi wa mara kwa mara, lakini tofauti na hapo kiukweli ni mchezaji ambaye anastaili pongezi kutokana na muda wake mwingi kuipigania Simbahadi kupewa cheo hicho cha unahodha," amesema Kajuna.
Kiongozi huyo amesema timu ipo kwenye mpango wa kusajili beki mwingine mwenye uwezo wa kuziba nafasi ya Mwanjali ambaye atakuwa na umri mdogo ambaye ataendana na ushindani waligi kwa namna ulivyo hivi sasa.
Amesema Simba inaelekea kwenye hatua ngumu ya kushiriki michuano ya kiataifa hivyo nilazima iwe na wachezaji wenye nguvu na uwezo wa hali ya juu wasiokusekana kwenye mechi zaidi ya tatu kutokana na majeruhi ya kawaida.
Mwanjali amejiunga Simba msimu uliopita akitokea kwao Zambia, na aliweza kucheza kwa uwezo mkubwa msimu uliopita na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi pia aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la FA.