STORY MJUKUU WA MSUKULE SEHEMU YA 3 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 10, 2017

STORY MJUKUU WA MSUKULE SEHEMU YA 3

STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
SEHEMU YA{3}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Share na marafiki www.hadithimtandaoni.blogspot.com
Kadri muda ulivyozidi kwenda pia ile mvua nayo ilizidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu.mara mawe ya barafu yakaanza kuanguka kutoka angani, hapo ndipo watu wakaanza kushtuka kutoka usingizini, sauti zikasikika zikitoka majumbani mwa wanakijiji wakishangilia kua mvua imenyesha. M zee zagamba na mkewe wakawa wamesimama mlangoni huku Wakimulika kwa tochi jinsi ile mvua ilivyokua ikinyesha kwa kasi kubwa ambayo haijawahi kushudiwa pale kijijini.
Mawe makubwa ya barafu yalianza kuanguka yakawa yanavunja paa za nyumba za wanakijiji,pia mazizi ya ng’ombe na mifugo mingine yakawa yanaharibiwa vibaya na yale mawe ya ajabu yaliyokua yakiletwa na ile mvua. Mifugo ikawa inakufa kama utitiri uliowekewa sumu kali, nyumba nyingi zikazidi kuteketea kwa maji kujaa ndani pia mawe kuvunja vunja zile nyumba mithiri ya biskuti inapoingia mdomoni mwa mtu ambae ana njaa ya siku mbili. Mvua ikazidi kuongezeka bila kukatika wala kupunguza, watu wakazidi kutapatapa huku na kule kila mmoja akawa anafanya kila awezalo ili kunusuru uhai wake, kina mama na watoto wadogo wakawa wanaangukiwa na yale mawe makubwa ya barafu, wakawa wana kufa kama kuku wenye ugonjwa wa kipindu pindu. Hali ikawa mbaya hadi majira ya saa kumi na moja alfajiri ambapo mvua uilitoweka kabisa, ikafika asubuhi mida ya saa kumi na mbili, mitaa ya kile kijiji ikaonekana ikiwa imejaa mizoga ya kuku,ng’ombe,mbuzi pamoja na wanyama wengine ambao walikufa kutokana na kuangukiwa na yale mawe pia kuzidiwa na wingi wa maji.
Hali ikawa ni ya kusikitisha zaidi pale ambapo miili ya watoto waadogo ilipoonekana ikiwa chini huku wengi wao wakiwa wamepondwa vibaya na yale mawe, watoto wengi wakaonekana wakiwa wamepoteza uhai, pia wanawake kadhaa nao waliokotwa wakiwa wamesombwa na maji…….(je nini kitatokea???? Usikose sehemu ya4) usikose kutembelea bog hii. Wajulishe marafiki kwa kushare blog ya www.hadithimtandaoni.blogspot.com}.
®HadithiMandaoni.blogspot.com
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();