HOT STORY: MJUKUU WA MSUKULE PART(17) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 29, 2017

HOT STORY: MJUKUU WA MSUKULE PART(17)

                                               STORY: MJUKUU WA MSUKULE(PART17)
                                               MWANDISHI: Amany Zabranco        
                                                Blog mainfo93.blogspot.com.
                                                Social media pages, fb.com?Maino93.instagram.com/Mainfo93, 
                                                Twitter.com/Mainfo93
                                              








Watu wakashikwa na butwaa kusikia  ile kauli, minong`ono ya hapa na pale ikashamiri huku wengi wakidai kuwa `saguda` itakuwa kachukuliwa msukule ama ndondocha. Wazee wa kimila ikabidi wamuombe yule mtaalamu kama ana uwezo basi amrudishe marehemu. Yule mtaalamu
akawaambia waende kwenye chumba alichokua analala marehemu halafu waweke dawa kwenye pembe au kona ya mlango. Haraka haraka wakaenda kufanya hivyo ghafra sauti ikasikika kwa mbali  `jamaniiiiiiii mi naendaaaaaa wamenichukuaaaaa!!!!!!`. Yule mtaalamu akasema kuwa bahati mbaya wamechelewa na tayari kisha chukuliwa na wachawi.

Ule msiba ukajawa na utata sana, wanakijiji wakawa wamebaki njia panda kuhusu ule msiba, watu wa dini wakapinga ile kauli ya mzee wa jadi, wakadai kuwa mungu ndiye aliyechukua roho ya marehemu na siyo nguvu za giza kama wao wanavyodai.
Watu wa dini wakaomba waizike ile maiti ili kutimiza lemgo la msiba.
Mzee zagamba na mkewe sarafia wakawa na wasiwasi mkubwa kuwa huenda bibi kiskiki cha mpingo kalipiza kisasi kutokana na kile kitendo cha kumfukuza pale kijijini.

Baada ya msiba kuisha, ndoto za ajabu zikawa zinamtokea sarafia akawa anaota kwamba mwanae karudi pale nyumbani na anamsimulia  jinsi alivyokuwa akiishi kuzimu. Kwa upande wa kule gamboshi alipokuwa saguda, walinzi wakaingia kwenye kile chumba cha misukule alipokua kawekwa saguda, mlinzi mmoja akasema ''sasa  huyu lazima akakatwe ulimi kama sheria za gamboshi yetu zilivyo''.

Wakamchukua tena saguda ili kumpeleka chumba cha kukatia ulimi, akawa anapiga kelelele lakini wakamshika kwa nguvu kisha mmoja wao akaja na kifaa cha kukatia ulimi kikiwa kimefunikwa kitambaa chekundu. Kwanza kabla hajamkata ulimi akampa saguda kipande cha kidole cha mtu ili akile, lakini saguda akageuza mikono kwa nyuma ili kupokea kile kipande cha kidole, wale walinzi wakakasirika sana kwa kuwa kile alichokifanya saguda kugeuza viganja vya mikono kwa nyuma ni moja kati ya makosa makubwa  katika ile gamboshi.

Wakamshika saguda wakamfunga kamba kisha wakamlaza chali juu ya meza kubwa iliyokuwa imetapakaa damu na vipande vya nyama za watu, mlinzi mmoja akashika kile kifaa cha kukatia ulimi, akaushika ulimi wa saguda, ghafra.........................(je kitatokea nini???? usikose part 18, ingia mainfo93.blogspot.com utapata kinachoendelea)

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();