MJUKUU WA MSUKULE PART (9) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 15, 2017

MJUKUU WA MSUKULE PART (9)

STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{9}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
                     Karibu sana mdau ujipatie mastory kila siku tembelea www.mainfo93.blogspot.com


Sehemu iliyopita tuliishia pale saguda alipokua akimsikiliza nyamizi akisimulia, sasa songa nayo mdogo mdogo

Nyamizi akendelea kusema “kwanza kabisa nilianza kwa kutembea na mwanaume ambaye aliniahidi kua atanipa pesa nyingi endapo nitampa penzi bila kutumia kinga, nakumbuka aliniambia kua hua anapata raha sana anapokula embe bila kumenya maganda”, akatoa shilingi elfu hamsini kisha akanipa mkononi akasema  hiyo ni kama zawadi tu, akasema mtonyo mwingi atanipa endapo nitamruhusu kuogelea kwenye kisima changu bila ya kutumia mtumbwi. Kweli nikajawa na tamaa nikamtimizia haja yake ili nipate pesa nyingi”.

        Saguda akiwa amekaa mkao wa kula kana kwamba anasoma stori nzuri za zabranco, saguda akasema “endelea kutiririka dada nyamizi!!”.

           Nyamizi akasema “baada ya siku kadhaa mvulana ambaye nampenda kwa dhati nae akaniomba nimfurahishe bila kutumia kondom!, kwa kua penzi langu kwake lilikua ni la kutoka moyoni nikaona ni hiyana kuacha kumfurahisha mtu ambaye ananipa faraja daima, nikaamua kumpatia ili akate kiu ya moyo wake”.

       Saguda akasema “kwa hiyo wewe hukuona haja ya kutumia kinga?”.

        Nyamizi akajibu “hapana wengi niliotembea nao ilikua tunatumia kinga, ila Yule mvulana ndie ambaye tulikua tukifanya nae bila ya  kutumia password kwa mda mrefu, baada ya mda mwingi hatimaye akafanikiwa kutikisa nyavu ya goal na kunipatia mimba. Nyumbani baba na mama hawakufurahishwa na kile kitendo wakadai kua ni kinyume na mila na maadili ya jamii hapa kijjijini, wakaniambia kwa ukali kua aliyenipa mimba ndio nije kuishi nae”.

        Saguda akasema “enheee!! Endelea kusimulia dada”

          Nyamizi akasema “Yule mvulana nikamfuata na kumueleza lile jambo, lakini akanikana na kusema kua yeye sie aliyenipa hiyo mimba. Nikabaki nimeduwaa kama bata aliyekoswa kugongwa na baiskeli huku nikiwa siamini kama kweli yeye ndiye kasema yale maneno, nikamuita Shija, shija, shijaaaaaa!! Lakini hakuitika akaanza kuondoka, nikalia sana kwa kua sikua na pa kwenda kukimbila na ujauzito wangu. Nikarudi nyumbani kuwaeleza wazazi, wakasema lazima watume watu waende kumkata Yule kijana, baba akakasirika akasema ‘ndoho gete nakoweja kozunya bhakenangole umwana wise halafu bhamleke!!ndoho ngete”.

Saguda akasema “je huyo shija walifanikiwa kumkamata??”.
Nyamizi akajibu “hamna hawakumpata kwa kua kipindi wanaenda kumfuata aliwahi kupata habari akatoroka hapa kijijini” na………..(je itakuaje mbeleni????/ usikose hapa ndo story inaanza kunoga, huko mbele utasisimka sana usikose kuja mainfo93). LEO MDAU WANGU NAKUOMBA SHARE www.mainfo93.blogspot.com kwenye whatsapp,facebook,insta,na twitter

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();