STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{10}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Karibu
sana mdau ujipatie mast0ry kila siku tembelea www.mainfo93.blogspot.com
Saguda
akasema “je huyo shija walifanikiwa kumkamata??”.
Nyamizi
akajibu “hamna hawakumpata kwa kua kipindi wanaenda kumfuata aliwahi kupata
habari akatoroka hapa kijijini”.
Saguda akasema “ikawaje?”
Nyamizi akajibu “ikabidi nitafute
mwanaume mwingine wa kunioa,lakini kila niliekua nampata aliishia kunichezea na
kuniacha,japokua uzuri wangu ulikua unawavutia wengi. Mwishowe nikaja kupata
huyu mume wangu ambaye ninaye sasa , yeye alikua ni kijana mpole sana pia alikua akijituma
sana katika kilimo cha mazao ya biashara, hivyo moyo wangu ukavutiwa nikawa
namfuata kumuelezea hisia zangu, lakini kwa kua tayari nilikua nimesha zaa mtoto
ikawa ni vigumu kwake kunikubalia”.
Nyamizi akaendelea kusimulia “Akawa
ananikatalia huku akisema kua yeye hayupo tayari kuoa inabidi nitafute mwanaume
mwingine, nikambembeleza lakini akakataa kabisa, ndipo nikampata tajiri mmoja
ndio akawa ananisaidia matumizi, kumbe
alikua ni muathirika wa ukimwi. Mimi bila ya kujua hili wala lile nikajua
nimepata mtu wa kunioa, akawa ananipa vitu vya gharama, siku moja akaniambia
tukutane kwenye lodge ya “Honey moon lodge” nikakubali siku hiyo nikajiandaa
vizuri , nikawa najipamba ili azidi kunipenda. Nikaanza safari hadi sehemu
Fulani,mara simu ikaita nilipoangalia nikagundua kua ni Yule mwanaume,
nikapokea kwa haraka”. Akaniuliza nimefika wapi nikamueleza akasema nimsubiri
pale anakuja kunipitia, baada ya dakika kadhaa ikaja gari karibu yangu ikapaki
akashuka Yule mwanaume nikamkimbilia na kutaka kumkumbatai lakini kwa mbali
nikamuona huyu mume wangu wa sasa roho ikanisuta nikaacha kumkumbatia Yule
mwanaume, huyu mume wangu akawa anapita nikaona nibora nimuache huyu tajiri
nikamkimbilia huyu mume wangu nikafika mbele yake nikamshika mkono, Yule tajiri
akawasha gari akaondoka kwa hasira. Nikapiga magoti chini na kumuomba huyu mume
wangu anikubalie kwa kua nilimpenda sana kutokana na tabia yake. Kweli siku
hiyo akanikubalia hadi akafikia hatua ya kunioa baada ya siku kadhaa.
Saguda akasema “nini kikafuata?”.
Nyamizi akasema “kwa kweli huyu mume
wangu alinipenda na kunijari sana; alikua akinihudumia mimi na mwanangu kila kitu japo hakua ni
mwanae, lakini kumbe mimi nilikua tayari nisha ambukizwa virusi vya ukimwi na
wanaume niliotembea nao hapo zamani, hali yangu ikazidi kua mbaya sana nikazidi
kudhoofika, mume wangu nae nikawa tayari nimesha muambukiza bila mimi kujua,
nilijisikia vibaya nikajua nimeua kiumbe kisichokua na hatiya kwa kua mume
wangu alinipenda sana. Hadi leo naishi na virusi vya ukimwi mimi na mume wangu
na tunatumia dozi”……….itaendelea zidi kuifatilia upate uhondo)