STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{14}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Karibu
sana mdau ujipatie mast0ry kila siku tembelea www.mainfo93.blogspot.com
Mara bibi yake naye akavua nguo kichawi
akawa uchi kisha akasema “mkuu Yule kijana ambaye atarithi mikoba yangu ndio
huyu nimemleta”. Yule mkuu akacheka kwa sauti ya juu
“hahahahahahahahahahaha....” kisha akasema “sasa utakua umetimiza masharti ya
mizimu”.
Mkuu akawaamrisha walinzi wamsogeze
Yule kijana mbele yake ili ampe kiapo cha kurithi kiti cha bibi yake,
lakini saguda akakataa mbele ya mkuu
kuapa kua atarithi uchawi wa bibi yake. Yule mkuu akakasirika akasema “sasa
tunakupa adhabu ili ujifunze”. Mkuu akawaambia walinzi wamchukue na kumpeleka
chumba cha ‘MISUKULE’.Walinzi wakamchukua saguda kwa ajiri ya
kumpeleka chumba cha misukule.
Walipomfikisha mule ndani saguda hakuamini macho yake kuwaona watu aliokua akiwafahamu kua walisha fariki miaka
mingi iliyopita kumbe walikua bado wanaishi katika himaya ya kuzimu, wale
misukule walikua wakiishi katika hali ya mateso makubwa. Saguda akawa anaogopa
kuwasogelea wale misukule kwa kua walikua wanatisha sana huku nywele na makucha
yao yakiwa marefu sana pia nywele zao zilikua ni chafu sana. Wale misukule
wakawa wanaongea kama mabubu kwa kua walikua wamekatwa ulimi kila mmoja.
Kwa upande wa nyumbani kwa mzee zagamba
wanashangaa hadi mida ya saa saba mchana saguda bado hajaamka kutoka chumbani
kwake. Ikabidi mzee zagamba aingie ili kumuamsha lakini mzee zagamba akajawa na
hofu kwa kua hakusikia hata sauti ya kuhema, ikabidi amshike kifuani ili
kuangalia mapigo ya moyo, bahati mbaya moyo ukawa haudundi. Chozi na sura ya
huzuni ikamjaa mzee zagamba kwa kujua kua tayari mwanae kisha fariki.
Taratibu zagamba akajaribu
kunyanyua mkono wa saguda lakini ukawa umekakamaa, akamfunika vizuri na
kumfumba macho kisha akatoka nje ili akamueleze mkewe sarafia. Lakini
alipomuambia tu kuhusu ule msiba ghafla sarafia akastuka na kuanguka chini akazimia.
Mzee zagamba akaita majirani wa karibu wakaja kumsaidia kumchukua sarafia kwa
ajiri ya kumpeleka hospitali
Baada ya masaa kadhaa habari zikazagaa kijiji
kizima...(ITAENDELEA, USIPITWE)