STORY:MJUKUU WA MSUKULE PART (11) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 17, 2017

STORY:MJUKUU WA MSUKULE PART (11)



STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{11}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
                     Karibu sana mdau ujipatie mast0ry kila siku tembelea www.mainfo93.blogspot.com

                             
Ghafla saguda chozi la huzuni likazidi kutanda usoni kwa ugonjwa alioupata dada yake. Akampa pole dada yake kisha akampatia zawadi aliyokua kamletea toka mjini, nyamizi akafurahi sana kuona mdogo wake anamkumbuka japo kwa zawadi. Saguda akamuaga dada yake kisha akarudi nyumbani, alipofika akamkuta mama yake akamuuliza “umemuona dada yako?, hayo ndio matatizo yaliyomkuta na wewe ujihadhari sana na hii dunia ya leo inayozidi kumomonyoka kama kipande cha biskuti?”. Saguda akayatafakari maneno ya mama yake kisha akasema kua atajitahidi kuyazingatia.

         Baada ya siku kadhaa kupita saguda akawauliza wazazi wake kuhusu alipo bibi yake “kisiki cha mpingo”, kwa kua alikua akimpenda sana alipokua mdogo. Mzee zagamba akamueleza kila kitu kuhusu bibi yake huyo,lakini saguda akashangaa kua bibi yake anatuhumiwa kua ni mchawi sugu. Kwa kua alikua akimpenda sana alipokua mdogo.
Upande wa kule kwenye kijiji alichohamia bibi ‘kisiki cha mpingo’wanakijiji wakaanza kumchukia kutokana na tabia zake za kuwachezea majirani zake  kichawi  nyakati  za usiku. Siku moja bibi kisiki cha mpingo akiwa katika kazi zake za kuwanga, akaenda kuiba kichawi pesa za mauzo kwenye grocery Fulani,lakini kumbe mmiliki wa hiyo grocery alikua kajiimarisha katika mambo ya kishirikina.

      Yule mmiliki wa ile grocery asubuhi alipoamka akashangaa kumuona bibi kisiki cha mpingo akiwa kaganda huku kasimama akiwa uchi wa mnyama,Yule mmiliki akawaita watu waje kushuhudia lile tukio. Watu wakajaa kuja kumshangaa huku akiwa kaduwaa akiwa hana ujanja wa kujinasua pale, kina mama wakaona aibu wakaona bora wamfunge kanga kwa kua wanaume na watoto wengi walikua wakimshuhudia kisiki cha mpingo alivyokua uchi.
     Mkuu wa mila kwenye kijiji  hicho akawasili alipokuta umati wa watu ukiwa umemwagika kwa wingi wakiwa wanashuhudia lile tukio mithiri ya shooo ya fiesta. Mkuu wa mila akatoa amri kua inabidi wasimuongeleshe  Yule  bibi  kwa kua wakifanya hivyo basi watakua ni kama wamemruhusu ajinasue kwenye ile dawa iliyomnasa.Mkuu wa mila akamsogelea Yule bibi akampaka dawa ya kumzuia asitoweke kimiujiza kisha wakaanza kumuhoji maswali.


    Yule mmliki wa ile grocery akaanza kulalamika kua mapato anayouza hua yanapungua bila hata ya yeye kujua kua yamepotelea wapi, akaendelea kusema kwa jaziba kubwa kua kumbe ndo hua kuna mchezo mchafu hua anachezewa na wachawi kama bibi huyo. Aka………..(itaendelea)



'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();