STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{8}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Karibu sana mdau ujipatie mastery kila siku tembelea
www.mainfo93.blogspot.com
Sehemu
iliyopita iliishia pale saguda alipofika na zawadi kwa wazazi wake, sasa
tiririka nayo.
Wote wawili
wakawa ni wenye furaha huku wakipendezwa na zile zawadi toka kwa saguda.
Sarafia akasema “mwanangu saguda,sasa inabidi uende pale kwa dada yako nyamizi
ukamsalimie maana anaumwa sana siku hizi. Saguda akakubali kwenda kumsalimia
dada yake ambae alikua kisha olewa pale kijijini. Alipofika alishangaa kumuona
‘nyamizi’akiwa kakonda sana akamsalimia “dada za siku nyingi?, nyamizi akajibu
‘mbaya sana mdogo wangu saguda’. Saguda akatikisa kichwa kama ishara ya
kusikitishwa na hali ya dada yake kisha akasema “pole sana dada, mbona
umedhoofika hivyo?”,nyamizi akajawa na sura ya huzuni huku chozi likimtiririka
mithiri ya manyunyu ya mvua akajibu “mdogo wangu,haya maisha we yaache tu kama
yalivyo!!!!”.Saguda akauliza “ni nini kimekusibu dada yangu?”.
Nyamizi akajibu “yani ni story ndefu sana, kwani
toka nifeli shule, nikawa sina pa kwenda na maisha yakawa na ushawishi toka kwa
mabinti wenzangu ambao walikua wakiniambia kua ili nipate mambo mazuri inabidi
nitumie mwili wangu”.
Saguda akauliza “ikawaje dada??”,
Nyamizi akajibu “kutokana na hali duni ya
maisha pamoja na umasikini zikanifanya
nianze kuuza mwili wangu kwa wanaume ili wanipatie fedha ya kununua vitu vizuri
, tamaa ikazidi kunijaa nikawa nabadili nguo na viatu vya bei kali kila bada ya
wiki moja. Kutokana na uzuri wangu
wanaume wengi pamoja na vijana wa rika langu wakawa wananitaka kimapenzi, bila
ya kujua ninachokifanya ni hatari kwa afya yangu na kizazi changu”.
Saguda akaina misha kichwa chini akawa
anakumbuka hadithi za mtunzi mahiri aitwaye Amani zabranco akawa anahisi
anachoki hadithia dada yake ni kama vile anasoma kitabu cha zabranco kumbe ndo
yashamtokea.
Saguda akauliza “kipi tena ambacho ni
hatari dada nyamizi??”.
Nyamizi akajibu “ unapokua unaruhusu
kijiti kichome kidonda chako kinachowasha,utajisikia raha ya kuondolewa
muwasho, lakini iwapo kijiti kitakua ni cha mti wa mwiba mkali, basi maumivu
yatakayo kuja badae ni makali kuliko ile hamu ya kidonda kuwasha”.
Saguda akasema “una maanisha nini
dada nyamizi?”………{je nyamizi alijibu niniiiii???? Usikose part8 hapahapa
mainfo93)