STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART12) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 19, 2017

STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART12)




STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{12}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.

   

Wananchi wakasema lazima wamuadhibu huyo bibi hadi kufa. Lakini bibi kisiki cha mpingo aliposikia hivyo akazungusha macho yake kuashiria kuvuta nguvu za ziada ili kujaribu kuepuka kifo. Mara ghafla kimbunga kikali kikatokea katikati ya wananchi, watu wakaanza kukimbia huku wakipiga mayowe kwa kuogopa kile kimbunga kwa kua kilikua na kasi ya ajabu. Baada ya dakika kadhaa hali ikawa imetulia lakini tayari bibi kisiki cha mpingo akawa tayari kisha toweka kimiujiza,
Kisiki cha mpingo akaenda kutokezea kule kwa marafiki zake kwenye kijiji cha mzee zagamba,alipofika kwa rafiki yake yani mchawi mwenzake akakaribishwa kwa furaha kubwa kwa kua kisiki cha mpingo alikua na cheo kikubwa kwenye kikosi cha wachawi.
     Yule rafiki yake akauliza kuhusu nini kilichomsibu,akamsimulia jinsi alivyokutana na dawa kali hadi akanaswa na wananchi. Rafiki yake akamuambia kua Yule mjukuu wake mtoto wa mzee zagamba ambaye ni saguda aliyekua masomoni tayari kisha rudi pale kijijini. Bibi kisiki cha mpingo akafurahi sana akasema “huyo kijana nimempenda sana tokea udogo wake, nataka awe ndio mrithi wa kiti changu kule gamboshi. Kisiki cha mpingo akasema sasa ndio wakati muafaka wa kulipiza kisasi kwa mzee zagamba kwa kumchukua mtoto wake huyo anayempenda ili ampeleke gamboshi.

      Kisiki cha mpingo akaendelea kukaa pale kwa rafiki yake huku akiwa hatoki nje ili wanakijiji wasiweze kumuona, baada ya wiki kadhaa kupita siku moja bibi kisiki cha mpingo akiwa anaongea na Yule rafiki yake, akamuambia kua leo ndio siku ya kumpeleka saguda kule gamboshi ili akapate kiapo cha kurithi kiti cha uchawi.

    Rafiki yake akafurahi akamuuliza ni njia ipi ataitumia ili kufanikisha hilo suala, akamjibu kua atatumia njia ya kuotesha ndoto ili akubali kumfuata. Kwa upande wa saguda jioni akiwa anaongea na wazazi wake kua zimebaki siku kadhaa ili arudi mjini kwenda kusaini mkataba wake wa kwanza wa kikazi kwa kua tayari alikua  kishahitimu  elimu yake ya chuo kikuu. Huku yeye akiwa hajui hili wala lile kumbe tayari alikua kawekewa mipango ya kwenda kurithi kiti cha bibi kisiki cha mpingo.

     *Usiku ‘saguda’ akiwa amelala mara akaota  ndoto ya ajabu kua Yule bibi yake ‘kisiki cha mpingo’anamuita waende kuchimba mizizi ya dawa polini,kutokana na kupoteza fahamu za kawaida saguda akaamka huku akiwa usingizini akaanza kuifuata  ile sauti ya bibi yake iliyokua ikimuita kuelekea porini. Alipofika njia panda ghafla akapotea kimiujiza………(je kitatokea ninii?/ usikose part13) INGIA WWW.MAINFO93.BLOGSPOT.COM



'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();