MJUKUU WA MSUKULE(PART15) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 24, 2017

MJUKUU WA MSUKULE(PART15)



STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{9}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.

Karibu sana mdau ujipatie mastOry kila siku tembelea 
www.mainfo93.blogspot.com


Baada ya masaa kadhaa habari zikazagaa kijiji kizima kua kwa mzee zagamba kuna msiba wa mwanae.Siku iliyofuata ikawa ndio siku ya mazishi Watu wakazidi kumiminika kuelekea kwa mzee zagamba kwa ajiri ya mipango ya mazishi. Baada ya muda kidogo gari likaonekana likija taratibu pale kwenye msiba huku watu wakiwa wana huzuni, akashuka sarafia akiwa kashikwa mikono na kina mama wenzake huku akitembea taratibu na chozi la uchungu likizidi kumiminika  mithiri ya maporomoko ya maji.

   Sarafia akapokelewa hadi ndani huku wanakijiji waliohuduria pale wakawa wamejawa na simanzi, watu wakazidi kushamiri kwenye msiba ule mda wa chakula ukafika, wanawake wakawa tayari wamepika chakula pale msibani huku wengine wakiwa wamekuja na vyakula toka majumbani kwao kama ilivyo  mila na desturi ya watu wa kile kijiji, wanawake wakavikusanya vile vyakula walivyovileta pale msibani ili watu wale. Kisha wakaanza kwenda kutenga kwenye vikundi vya watu waliokua wamekaa pale  nje, wakaanza na upande wa wanaume.

   Wanaume walikua wakiendelea kupiga stori za hapa na pale huku wengine wakiwa wanacheza karata. Chakula kikatengwa watu waanze kula makundi mengine yakaanza kula,wakati makundi hayo yanaendekea kula kuna kundi moja ambalo lilikua na mzee wa mila walipotaka kuanza kula kwenye lile kundi, mmoja wao alipofunua bakuri moja la mboga akashangaa kukutana na nyoka mweusi akiwa amejikunja ndani ya lile bakuri.
Wote wakasambaa kwenye kile kikundi kwa kumuogopa Yule  nyoka.Sauti za minong’ono zikazidi kusikika kutoka kwa wanakijiji waliokua pale msibani.


      Mkuu wa mila ikabidi amuite kiongozi wa kina mama ili kubaini lile bakuri lenye Yule nyoka ni la nani,wakaitwa na wanawake wengine watatu wakasema lile bakuri ni la mama mmoja aitwaye ‘chaubishi’.Wale wazee wa kimila wakamuamulu Yule mwanamke aitwe pale mbele ya hadhara ili atoe maelezo ni kwa nini chombo chake pekee ndo kimeonekana na kasoro. Walipomfikisha watu hawakukubali aendelee kuishi pale kwa kuwa alikua ni mmoja wa wanawake watatu  ambao wawili  walikua wazee naye pekee ndio alikua  kijana. Huyu mwanamke aliwahi kuvunja amri ya kuongea na kisiki cha mpingo.


    Mkuu wa mila akamuuliza kuhusu Yule nyoka ndani ya bakuri, lakini akajibu kua hafahamu ametokea wapi Yule nyoka. Wanakijiji wakakasirika wakasema apewe adhabu ya viboko vya nguvu ili liwe funzo kwa wengine. Akaambiwa amchukue Yule nyoka ampinge hadi..(ITAENDELEA USIKOSE)
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();