STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART13) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 20, 2017

STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART13)




    STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{13}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
                     Karibu sana mdau ujipatie mastory kila siku tembelea www.mainfo93.blogspot.com



Baada ya saa kadhaa akajikuta fahamu zinamjia akajikuta akiwa katikati ya pori nene huku bibi yake kisiki cha mpingo akiwa kamshikiria mkono. Saguda akajitutumua kwa nguvu akafanikiwa kumponyoka bibi yake kisha akaanza kukimbia mule porini huku akipiga kelele , akakimbia hadi kwenye kichaka Fulani, bahati mbaya akakutana na fisi mnene mweusi, Yule fisi alikua anatoa ulimi wake huku ukiwa unatoa udenda kuashiria kua ana hamu na nyama ya binadamu, saguda akazidi kuchanja mbuga kama husein bolt, lakini wakati anakimbia akajikwaa kwenye kisiki, kipande cha mti kikamchoma mguuni damu ikawa inamtoka sana, wakati saguda anajaribu kuuchomoa ule mti Yule fisi akazidi kuja kwa kasi.
   
    Saguda akafanikiwa kuuchomoa ule mti kisha akaanza kukimbia huku akichechemea mguu, saguda akazidi kuelemewa na maumivu ya lile jeraha la mguuni, akajikuta ameanguka chini, lakini aliponyanyua macho yake juu ili asimame akajikuta akiwa chini ya miguu ya bibi kisiki cha mpingo.
 Yule bibi akaanza kucheka kwa dharau huku Yule fisi akawa amekaribia kufika pale alipoanguka saguda, Yule bibi akanyoosha mkono wake kuelekea kwa Yule fisi ghafla mkono wa kisiki cha mpingo ukatoa cheche ambazo zikamuua Yule fisi.


      Saguda  alipoona  vile  akataka  kukimbia tena ila miguu ikawa  haina nguvu, akawa kila akitaka kukimbia anajikuta yuko pale pale akawa anahisi miguu ni mizito kama vile imefungwa minyororo. Mara kisiki cha mpingo akamshika mkono na kupotea nae ghafla.
Baada ya dakika kadhaa saguda akajikuta akiwa kwenye barabara kubwa mule porini akataka kupiga kelele lakini sauti haikuweza kutoka. Kwa mbali akaona gari likija taratibu, bibi yake akamwambia kua usafiri ndio umefika kuwachukua. Lile gari lilipo karibia pale walipokua likawasha taa kuashiria kuwaruhusu ili waingie kwa ajiri ya kuendelea na safari. Lilipo karibia zaidi akashuka mtu mmoja wa ajabu akiwa na nywele ndefu na makucha marefu akawaambia waingie ili waondoke. Saguda akawa anakataa kuingia lakini Yule mtu akamshika kwa nguvu na kumtupia kwenye gari.
Kisiki cha mpingo  naye  akaingia, lakini saguda bado akataka kupiga kelele ila kisiki cha mpingo akampaka dawa mdomoni ili asiweze kutoa sauti. Kila saguda akitaka kutoa sauti haitoki. Baada ya mda kidogo  gari likakaribia  eneo ambalo kwa mbali saguda akawa anaona majengo mazuri yakiwa yamepanda juu kwa ghorofa ndefu sana, saguda akawa anashangaa kwa kua lile eneo alikua akipita nyakati za mchana haoni nyumba yoyote.
   Gari lilipokaribia zaidi bibi kisiki cha mpingo akawaambia wale watu waliokuwa kwenye lile gari ambapo wote walikua uchi wa mnyama huku nywele na kucha zikiwa ndefu sana,bibi kisiki cha mpingo akasema. “sasa tumefika kambini kwetu, gamboshi la magamboshi yote”. Saguda akastuka kusikia neno gamboshi kwa kua habari zake alikua akizisikia na kuzisoma sehemu mbalimbali lakini leo anapelekwa sehemu hiyo. Gari lilipopaki watu wakaanza kushuka lakini saguda akawa mbishi bibi yake akamvuta kichawi hadi chini.


     Mara  saguda akajikuta akiwa chini ya mti mkubwa wa mbuyu ambapo alishangaa kuona watu wengi wote wakiwa uchi huku ndugu zake wa kule kijijini pamoja na watu wengine anaowajua akawaona…………(Itaendelea, usikose kuifatilia kwa kuingia www.mainfo93.blogspot.com
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();