WWW.MAINFO93.BLOGSPOT.COM.
Kutoka bungeni dodoma, swali lililoulizwa na mbunge wa Newala (George Mkuchika), aliuliza juu ya suala la mafunzo ya jkt kwa mujibu wa sheria kuonekana kupungua idadi ya wanafunzi wanaojiunga.
Akijibu swali hilo, waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dk,Hussein Mwinyi alisema kuacha rasilimali fedha mbalimbali kuna changamoto nyingi zinazopelekea kupungua kwa idadi hiyo.
Dk mwinyi akataja kugongana kwa tarehe rasmi za kuanza mafunzo hayo pamoja na zile za kufungua vyuo vikuu.
Akiendelea kutolea ufafanuzi, Dk mwinyi akasema mwaka 2016 idadi ya vijana waliomaliza kidato cha sita walikua ni 40,753 lakini waliojiunga na jkt walikua 19,990 sawa na asilimia 48.8. Mwinyi akasema mwaka huu waliochaguliwa ni 14,747 sawa na asilimia 23.2 kati ya 63,623 waliohitimu kidato cha sita mwaka huu 2017
Naye mbunge Willfred Lwakatare akauliza kuwa ni vigezo gani serikali inavitumia ili kuchagua baadhi watakaojiunga na jkt na wale wanaobaki.
Akijibu swali la Lwakatare, mwinyi alisema hakuna vigezo vinavyotumika kuwachagua na kuwaacha baadhi, mwinyi akaendelea kusema kuwa hua inafanyika Random selection.
USIKOSE KUJA MAINFO93 HAPA UTAPATA MAINFO UNIQUE UTAZANI SI YA NCHI HII.