STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART(18)
MWANDISHI: Amani Zabranco
Mainfo93.blogspot.c
fb page facebook.com/Mainfo93
Mara ghafra akaingia bibi kizee mmoja kwenye kile chumba cha
kukatia ulimi,huku akiwa amevaa nguo kubwa nyekukundu mithiri ya joho la spika
wa bunge. Yule bibi akawaambia wale walinzi
‘’niachieni huyu nimshughurikie
mimi mwenyewe’’, wale walinzi wakaondoka akabaki saguda na yule kikongwe, kisha
yule bibi akamtoa saguda pale walipokuwa wamemlaza kwa ajiri ya kumkata ulimi.
Bibi kizee akaanza kumuuliza saguda kuwa ni kivipi
amefika kwenye hiyo ngome ya gamboshi??. Saguda akamsimulia jinsi ilivyokuwa kisha yule bibi akaanza kutikisa kichwa kwa kumuonea huruma saguda,yule bibi akatokea
kuguswa na mateso anayoyapata saguda,akamuahidi kua atamsaidia mbinu za
kutoroka kutoka kwenye ile gamboshi, yule bibi akasema
‘’kuanzia leo wewe jina lako ni mjukuu wa msukule kwa kuwa hilo jina lina nyota kari itakayokusaidia kupambana
na wachawi hadi kutoroka’’. Yule bibi akazidi kumuahidi saguda kuwa atamlinda ili asikatwe ulimi kama misukule wengine,
kikongwe akamchukua saguda na kumpeleka kwenye jengo alilokuwa akiishi yeye
pale gamboshi. Usiku ulipofika yule bibi akaanza kumsimulia saguda jinsi nguvu ya
kishetani inavyotumiwa na watu wengi.
Yule bibi akaanza kusema kwa sauti nzito iliyokuwa ikijirudia mara mbili mbili ‘’mjukuu wangu
binadamu wengi wenye mapesa na umaarufu katika jamii wanategemea sana nguvu za
miujiza ili kufanikisha mambo yao. Pia wafanya biashara Zaidi ya asilimia 85%
wanatumia nguvu za giza ili kuvutia
wateja’’.
Yule kikongwe akaendelea kusema ‘ndio maana uchawi hauwezi kushuka nguvu miaka mia nane’’. Saguda
akavutiwa na maneno ya yule bibi kisha akauliza ‘je wewe ulianzaje kufanya hii kazi mbaya kabisaa???.
Yule bibi akamjibu kua ‘’nilifundishwa
uchawi na shangazi yangu miaka mingi iliyopita, lakini sipendi na wewe mjukuu
wangu uingie kwenye hii
kazi ya kumuasi mungu’’.
Yule bibi alipotaja neono mungu, saguda akastuka akamuuliza ‘’je na wewe
bibi unaamini mungu???’’. Yule kikongwe
akajibu ‘’napenda sana mtu anaye amini mungu, kwa kuwa hata mimi nilikuwa ni
muimbaji wa kikundi cha kwaya kanisani, nampenda mtu anayeamini mungu kwa kua
huweza kuleta Amani, upendo na umoja katika jamii, lakini wachawi huleta
chuki,fitina, kuua watu wasio na hatia pia huwa ni kikwazo cha maendeleo katiaka
jamii’’.
Saguda akauliza…………………(ITAENDELAAAA!!!!)