STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
PART{7}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Mkuu wa mila
akatoa amri kua wale wanakijiji watatu wapigwe viboko mbele ya wanakijiji ili liwe funzo kwa yeyote
atakayekiuka makubaliano ya mkutano. Wakati wakisubiri kisiki cha mpingo
aletwe, adhabu ya viboko ikazidi kutolewa kwa wale wanawake watatu.
Mara gari la aina ya ‘kenta’ likaonekana
likija taratibu pale kwenye mkutano
likiwa limebeba mizigo ya bibi kisiki cha mpingo. Akawekwa chini mbele ya wanakijiji
kisha mzee zagamba akamuambia kuwa inabidi atoweke haraka pale kijijini. Wanakijiji
wakafurahi kusikia kauli hiyo, bibi kisiki cha mpingo akachukuliwa na walinzi
akaingizwa kwenye gari kwa ajiri ya kusafirishwa. Baada ya miezi kadhaa kupita
huku kisiki cha cha mpingo akiwa kisha ondoka pale kijijini, neema ya mvua
ikaingia , wanakijiji wakalima mazao yao na kuvuna kwa wingi sana.
Siku moja
mzee zagamba akiwa amekaa nje akifurahia hewa safi itokayo kwenye miti mizuri
iliyokua kando ya nyumba yake,mara kwa mbari akamuona kijana karibia na
nyumbani kwake. Alipokaribia kumbe alikua ni mwanae wa kiume aliyekua masomoni.
Mzee zagamba kwa shauku akamuita mkewe ‘sarafia’ aje kumpokea kijana wao
mpendwa. Sarafia alipotoka nje hakuamini macho yake kumuona mwanae kipenzi
karudi nyumbani , kwa shauku akasema.
“Waaaaaaaawwww,karibu
sana baba angu” huku wakikumbatiana kwa hisia za kufurahia kuonana tena.
Sarafia akasema “mwanangu pole sana na masomo”. Kijana akajibu “ahsante ,mama
tayari nishapoa”. Mzee zagamba akadakia ‘mwanangu, wewe ndio jembe letu,kwa kua
unajituma sana sio kama wenzako kina choroko wao kazi yao kulima tu hapa
kijijini”.
Sarafia akamletea kiti mwanae ili akae kwa
ajiri ya kusalimiana na baba yake. Maongezi yakaendelea huku kila mmoja
akifurahia kumuona mwenzake kwa mara nyingine tena.Kijana Yule aliyekua
akijulikana kwa jina la ‘saguda’
akatoa zawadi ya simu za mkononi moja akampa baba yake na nyingine akampa mama
yake. Lakini mama akasema “mwanangu hii simu mbona ni kama kioo cha
kujiangalia?”,saguda akatabasamu kisha akajibu “Aaaaahhh.....mama hiyo inaitwa
smartphone au screen touch”. Mama akatabasamu akasema “inabidi tupeane cozi ya
namna ya kuitumia kwa sababu mimi na baba yako hatujawahi kuona simu kama hizi!”.
Mzee zagamba akadakia “mimi mbona dakika hii tayari nisha anza kuielewa,
ona hapa nagusa kidogo tu kwa kidole
yanakuja matufe mengi mengi, sema ndo sijaelewa yana maaisha nini”. Mama
akadakia kwa kusema “nahisi moja hapo litakua ni la ile wanaitaka facebook”…………..(itaendelea)
usikose kutembelea mainfo93