STORY MJUKUU WA MSUKULE SEHEMU YA 2 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 10, 2017

STORY MJUKUU WA MSUKULE SEHEMU YA 2

STORY:MJUKUU WA MSUKULE.SEHEMU YA{2}.MWANDISHI:#Amani zabranco.Share na marafiki www.hadithimtandaoni.blogspot.com
Mtaalamu wa kwanza, akarusha koti lake juu kisha akaliaamrisha lile koti ligande hewani, kweli lile koti likabaki limening’inia hewani. Wote wakapiga makofi kama ishara ya kumpongeza Yule mtaalamu kwa jinsi alivyoonyesha uwezo wa hali ya Juu.
Mtaalamu wa pili yeye akaiamrisha mvua inyeshe pembeni kidogo ya pale walipokua wamesimama, mara ghafla manyunyu ya mvua yakaanza kudondoka. Nae wakampongeza kwa ngoma na makofi mazito mithiri ya wabunge walioshiba makande.
Sasa ikafika zamu ya mtaalamu wa tatu, yeye akaamrisha mkuki wake ambao upo nyumbani kwake amabao hua anautumia kwenye kazi zake,akatamka maneno kuwa ule mkuki utoke nyumbani kwake na utue pale walipokua wamesimama, kweli baada ya sekunde kadhaa kimbunga kikali kikaonekana kikijongea kuelekea pale walipokua wamesimama, mara ghafra kile kimbunga kilipofika pale walipokua kikatoweka na mkuki ukaonekana ukiwa umesimama, Yule mtaalamu akauchukua mkuki wake kisha akaubusu akacheka kwa sauti ya juu huku akipiga piga kifua chake kuonyesha kua yeye ndo yeye. Wote ikabidi wampigie ngoma huku wakimpigia makofi kisha wote wakacheka kwa sauti ya juu mithiri ya jambazi.
Mkuu wa mila akasema kua, sasa ni wakati wa kufanya matambiko akasema kua kwenye ule mbuyu kuna kichaka kidogo ambacho kuna chui mkubwa ambaye anaaminika kua ni mzimu, pia mkuu wa mila akasema katikati ya mti wa mbuyu kuna shimo lenye nyoka mkubwa ambao mzimu unaoogopeka sana na watu wengi kutoka kila kona ya kile kijiji pia hata vijiji vya jirani wanafahamu kua huo mzimu ni tishio kubwa.
Wale wataalamu wakaweka ngozi ya chui wakaitandika chini kisha wakachukua vibuyu vyao vyenye dawa ili waanze matambiko. Wakaamlisha damu ya Yule ng’ombe na damu ya Yule mbuzi isogezwe Ile damu ikaletwa karibu huku ikiwa kwenye vyungu viwili tofauti,kisha wakaanza kazi yao ya matambiko. Mara sauti za ajabu zikatanda eneo lile, huku wataalamu hao wakiendelea na kazi yao pale chini. Mara moto mkubwa ukatokea katikati ya lile shimo la mbuyu.
Mtaalamu mmoja akachukua chungu chenye damu ya ng’ombe akaumwagia ule moto ukazimika, huku kazi ya kutambika ikiwa inaendelea mara moto ukatokea kwenye kile kichaka kilichokua karibu na ule mbuyu. Mtaalamu akachukua chungu chenye damu ya mbuzi akaimwaga kwenye ule moto hatimaye ukazima.
Yule mkuu wa mila pale kijijini akawapongeza wale wataalamu kutoka kijiji cha “mizizi mitatu” kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha kua wanasaidia kufanya matambiko ili kutatua tatizo la mvua pale kijijini. Baada ya kumaliza kazi yao wakarejea nyumbani . Siku tatu zikapita baada ya yale matambiko kufanyika pale kijijini, siku ya tatu ikiwa ni majira ya saa sita usiku huku watu wakiwa wamelala ghafla hali ya hewa ikabadilika, radi na ngurumo zikatanda anga la kile kijiji.
Wingu zito likawa limetanda angani nje pakawa giza kama ndani ya shimo lisilopitisha hata chembe ya mwanga. Muda mfupi baadae mvua kali iliyoambatana na upepo mkali ikaanza kuyesha, watu wakiwa hawajui kinachoendelea wengi wao wakawa wamelala fofofooo. Ghafla………. Itaendelea,usikose kutembelea bog hii. Wajulishe marafiki kwa kushare blog ya www.hadithimtandaoni.blogspot.com
®Hadithi Mandaoni
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();