STORY: MJUKUU WA MSUKULE( PART1) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

May 11, 2017

STORY: MJUKUU WA MSUKULE( PART1)



STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
SEHEMU YA{1}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Share na marafiki www.hadithimtandaoni.blogspot.com

Miaka kadhaa iliyopita, kulikua kuna familia ya mzee “zagamba” ambayo ilikua ni familia ya kimila. Wana ukoo wengi kwenye ile familia  walikua  wakiongoza  jamii katika nyadhifa mbali mbali. Kutokana na mila za jamii hiyo, kuwa ukoo huo ulikuwa na hadhi kubwa katika ile jamii,pia kulikua na watu wenye uwezo wakufanya mambo mazito ya kimila kutoka kwenye ukoo ule.
    Siku moja “mzee Zagamba”akiwa nyumbani kwake, huku wakiwa wanazungumza na mkewe “sarafia”,kuhusu jinsi mambo yakifamilia yanavyoendelea kwenye ndoa yao. Mara wakatokea wageni watatu wakiongozwa na mkuu wa kimila pale kijijini. Mzee zagamba akamwambia mkewe achukue viti  vya kimila  ili  awapatie wageni  walioonekana kua ni watu wa kutoka kijiji jirani.
                  
      Akawaambia “karibuni sana”,Wazee wenzangu wote kwa pamoja wakajibu  “tunashukuru sana mzee zagamba”. Sarafia  akatoka  ndani na viti vitatu vyenye rangi tofauti tofauti. kimoja kilikua chekundu, kingine kilikua cheupe na kingine kilikua cha rangi  nyeusi. Kile chekundu akapewa mkuu wa mila pale kijijini  na vingine viwili wakapewa wale wageni. Hii ilikua ni sheria ya kimila  kwa watu wenye vyeo tofauti.

      Mazungumzo yakaanza, ila mzee zagamba akamuambia mkewe “sarafia”, awaletee vibuyu vya asali ili wabarikiwe na mizimu kabla ya maongezi yao kuanza. Sarafia akaleta vibuyu vilivyofungwa vitambaa vya rangi tofauti, kimoja chekundu,cheupe na cheusi kama alivyo  gawa viti kutokana na rangi. Hivyo hivyo ndo akagawa na  vile vibuyu vya asali. Kibuyu Chekundundu  akampa mkuu wa mila pale kijijini, na vingine akawapa wale wageni. Kisha sarafia akarudi ndani na kuwaacha waendelee  na mazungumzo.
Mzee zagamba akasema “nimefurahi sana kunitembelea nyumbani  kwangu, wote wakajibu ‘nasi  tumefurahi kwa mapokezi mazuri”. Mzee  zagamba akasema “mkuu wa mila nadhani,umekuja tujadiri lile suala la ukosevu wa mvua hapa kijijini”.
                    
      Mkuu wa mila akajibu ‘haswaaaaa!!!, hicho ndicho kilichonileta hapa kwako , na hawa unaowaona mbele yako ni wataalamu wa masuala ya  kafara kutoka kijiji cha mizizi mitatu. Mzee zagamba akatabasamu kisha akasema “nadhani huu ndo utakua mwisho wa balaa la mvua na ukame hapa kijijini”. Mazungumzo yakaendelea na wakakubaliana kua kesho yake usiku wa manane inawabidi waende kwenye  mti wa ‘mbuyu’, ambapo ndipo watakapofanyia  matambiko ya kijadi kwa kua ndio panaaminika kua pana mzimu  wenye nguvu za ajabu sana.

   Wote wakakubaliana  kua inawabidi waandae mbuzi pamoja na ng’ombe kwa kuzingatia  masharti, hao wanyama inatakiwa mmoja wao awe na rangi nyeupe na mwingine awe na rangi nyeusi kwa ajiri ya kafara.Wale wageni wakaondoka kuelekea  nyumbani kwa mkuu wa kimila  kwa kua ndipo walipokua wamefikia.  Walipoondoka wale wageni, mara sarafia akatoka nje akamfuata mumewe  akamuuliza kuhusu  majadiriano yao. Mzee zagamba akamjibu kua wanataka kutatua suala la ukosefu wa mvua pale kijijini hivyo basi wametafuta wataalamu wa masuala ya ‘kafara’ kwa ajiri ya kushunghurikia  hilo suala.

     Siku ile ikapita ,sasa  mzee ‘zagamba’ akiwa kisha andaa  ngozi ya chui pamoja na mbuzi. Kwa upande wa pili mkuu wa kimila alikua tayari kisha andaa  ng’ombe  toka kwa mfugaji aliyejitolea  kutoa  ng’ombe huyo ili kukinusuru  kijiji  kutokana na janga hilo la ukame.
Usiku ukafika kikundi cha watu kumi na mbili, akiwemo mzee zagamba kikafunga safari ya kuelekea kwenye ule mti wa mbuyu, kwa ajiri ya kwenda kufanya matambiko ya kuhakikisha kua mizimu inasaidia kurudisha  mvua  pale kijijini. Walipofika, kwanza wale wataalamu kutoka kijiji cha ‘mizizi mitatu’ wakaambiwa wafanye  kitu cha miujiza ili kuonyesha umahiri wao.

     Mtaalamu wa kwanza, akarusha koti lake juu kisha akaliaamrisha lile koti  ligande hewani,ghafra………………………….{Itaendelea,usikose kutembelea bog hii. Wajulishe marafiki kwa kushare blog ya www.hadithimtandaoni.blogspot.com}.
®HadithiMandaoni.blogspot.com

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();