STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
SEHEMU YA{4}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Share na marafiki www.hadithimtandaoni.blogspot.com
Familia ya mzee zagamba ilikua haijapoteza hata mtu mmoja kwa kua
mzee zagamba alikua na nyumba imara ambayo iliadhiriwa kidogo tu na ile
mvua. Mamia ya wanakijiji wakawa hawana nyumba kabisa kwa kua nyumba
zao zilivunjwa vunjwa na ile mvua. Watu hawakua hata na akiba ya chakula
kwa kua vyakula vyao vilisombwa na maji.
Mzee zagamba akawa anasikitika kwa kile kilicho kikumba kijiji chao. Mzee zagamba pamoja na mkewe ‘sarafia’wakawa wanajadidiliana kuhusu ujio wa ile mvua ambayo walitegemea iwaletee manufaa lakini ikawaletea balaaa kubwa ambalo halijawahi kutokea. Sarafia akasema “Mume wangu mimi nina jambo nalifikiria”. Mzee zagamba akauliza kwa tahaluki “enheeeee!!!! Jambo gani tena?. Sarafia akasema “mimi nahisi hii ni mipango ya bibi kisiki cha mpingo!, kwa kua yeye ndiye mchawi nguli hapa kijijini na anatupinga sana kwenye vikao vyetu vya maendeleo hapa kijijini!.
Mzee zagamba akainamisha kichwa chini huku akitafakari kauli ya mkewe kwani ina mlenga bibi ‘kisiki cha mpingo’, ambaye ni ndugu wa karibu wa mzee zagamba. Baada ya dakika kadhaa za kutafakari mzee zagamba akajibu “yaweza kua yeye ndio chanzo maana hata kwenye kikao cha kujadili suala la mvua kwenye mkutano mkuu wa kijiji huyu “kisiki cha mpingo”alitupinga sana”.
Sarafia akasema kua lazima watafute mbinu za kuhakikisha kua anahamishwa kijiji kwa kua wao wameshindwa kuishi nae kutokana na kua uwepo wake ni kikwazo cha maendeleo ya kijiji chao. Wote wawili wakakubaliana kuitisha kikao cha dharura kwa ajiri ya kutangaza rasmi kumtenga bibi ‘kisiki cha mpingo’ kutokana na uchawi wake.
Kesho yake kikao kikaitishwa ili kutoa tamko rasmi la ukoo wa mzee zagamba ambao unaheshimiwa na kijiji kuliko ukoo mwingine, kua wameamua kumtenga bibi “kisiki cha mpingo”. Mzee zagamba akasimama mbele ya umati wa wanakijiji waliofurika kwa wingi mithiri ya kuku waliomwagiwa punje za mtama. Ili kuweza kusikiliza kipi ambacho mzee zagamba anataka kuwaambia wanakijiji.Mzee ‘zagamba’akasema “kwanza kabisa ningependa kutoa pole kwa kila familia iliyokumbwa na janga hili la mvua ya ajabu ambayo hata mimi na uzee wangu sijawahi kushuhudia mvua kubwa kama hiyo tokea nizaliwe”.mzee zagamba akaendelea kuhutubia umati wa wanakijiji kwa kusema “Napia napenda kuwasihi wanakijiji wote mhakikishe kua mnatumia chakula kilichobaki kwa mipango mizuri ili kitosheleze tatizo hili,………….{itaendelea}