NIYONZIMA AFANYISHWA TIZI AKIWA ANAUMWA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 15, 2017

NIYONZIMA AFANYISHWA TIZI AKIWA ANAUMWA

Ili kuhakikisha anaitumikia timu yake kwenye mchezo ujao dhidi ya Prisons na kuondoka na alama zote tatu, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, jana amefanya mazoezi akiwa mgonjwa.
Niyonzima amefanya mazoezi hayo akiwa anaumwa homa ya matumbo (typhoid), wakati wakijiandaa na mechi ya Jumamosi ijayo dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Niyonzima alisema analazimika kufanya hivyo kutokana na kuwa na hamu kubwa ya kuisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu ili waendelee kukaa kileleni mwa ligi kuu.
"Nasumbumbuliwa na typhoid lakini nafanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Prisons, nataka kuona tunashinda ndiyo maana nimekuwa sehemu ya timu licha ya kuumwa kwangu.
"Kikubwa tunataka kuona hizi pointi tatu za Prisons tunazichukua zote kama tulivyofanya kwa Mbeya City," alisema Niyonzima.
Mbali na Niyonzima kusumbuliwa na ugonjwa huo, lakini pia James Kotei juzi Jumatatu alishindwa kufanya mazoezi kutokana na kuumwa, lakini jana alikuwa fiti.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();