- MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 13, 2017

Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
LICHA ya kufungwa mechi mbili mfululizo, Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameweka bayana kwamba ana uhakika mkubwa wa kucheza ligi kuu kwa
msimu ujao kutokana na kubakisha michezo mitatu yenye pointi tisa wakiwa nyumbani.
Dodoma FC juzi Jumamosi walipoteza mchezo wao dhidi ya Biashara Mara kwa bao 1-0, wakiwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ambapo kwa matokeo hayo yameifanya timu hiyo kuporomoka kutoka kileleni hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 18.
Julio ameliambia Championi Jumatatu kuwa atahakikisha anakiandaa kikosi chake kufanya vizuri kwenye michezo hiyo ya nyumbani ili iweze kuibeba timu yake na kupata pointi ambazo zitawafanya watinge ligi kuu.
“Sina wasiwasi kwamba tunapata matokeo mabaya kwa sasa baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo, kikubwa tunaamini kwamba tuna nafasi kubwa ya kutinga ligi kuu msimu ujao, tumebakisha mechi tatu kwenye uwanja wetu wa nyumbani, kwenye michezo hiyo najua kabisa tuna uhakika wa kupata pointi zote ambazo zitafanya mahesabu yetu yakamilike,” alisema Julio
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();