HIZI HAPA NCHI ZA AFRICA ZINAZOTENGENEZA MAGARI - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 19, 2017

HIZI HAPA NCHI ZA AFRICA ZINAZOTENGENEZA MAGARI

Karibu sana mainfo93.com

Siku hadi siku bara la Afrika linaendelea kuisogelea Teknolojia na kufanya vitu ambavyo tumezoea kuviona ni vya kawaida kwa nchi za wenzetu ambapo sasa kuna magari yanatengenezwa kwenye
nchi za Afrika.
KENYA
Nchi ya kwanza ni Kenya ambapo kampuni ya Mobius Motors ambayo ilianzishwa na Mwekezaji Muingereza mwaka 2009 inatarajia kuanza kuuza Mobius II mwaka 2018 na tayari wameshaanza kupokea oda, picha zake ndio hizi hapa chini.
Bei ya Mobius inaanzia Milioni 27 za Kitanzania.


Rekodi zinaonyesha kuwa Kenya haikuanza kutengeneza magari juzi, gari lao la kwanza lilitengenezwa mwaka 1986 na lilikua linaitwa Nyayo na ilikua ni kampuni ya Serikali lakini ikashindwa kuendelea.
UGANDA
Nchi ya pili ni Uganda ambapo magari yanatengenezwa na KIIRA MOTORS ambayo pia mpango wao ni kuleta aina mpya ya gari ya kutembelea mwaka 2018 tofauti na mwanzoni walivyoanza kwa kutengeneza Mabasi.
Inaripotiwa kwamba Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewekeza Dola za Kimarekani MILIONI 43.5
Basi kutoka Kiira Motors ambalo linatumia nguvu ya jua na linaweza kutembea umbali wa mpaka maili 50, ni basi lenye siti 35.
Kiira Motors Uganda
NIGERIA
Nigeria ni nchi ya tatu kwenye hii orodha ya nchi 5, wenyewe wanayo hii Innoson Motors iliyoanzishwa na Mnigeria Innocent Chukwuma ikiwa ni kampuni ambayo iliingiza sokoni magari kadhaa ya kutembelea mwaka 2014.
TUNISIA:
Namba 4 ni Tunisia ambao wana WallysCAR kampuni iliyoanzishwa mwaka 2007, ni gari ambalo lina siti mbili na linabeba injini ya Peugeot ambapo kwa mwaka inaingiza sokoni magari yasiyopungua 600.
GHANA:
Kampuni ya Kantanka inatambulika kama kampuni ya kwanza kutengeneza magari yenyewe Ghana, ni magari ambayo bei yake inaanzia milioni zisizopungua 40 za Kitanzania ambapo Jeshi la Polisi ni miongoni mwa Wateja wao wakubwa.
Tanzania imewahi kuingia kwenye headlines za kutengeneza magari yake ambayo yalipewa jina la NYUMBU yakitengenezwa na kampuni ya MZINGA ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania lakini ni muda sasa hatujasikia.
NYUMBU
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();