MKWASA AFUNGUKA INSHU YA KIPA KAKOLANYA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 17, 2017

MKWASA AFUNGUKA INSHU YA KIPA KAKOLANYA

Uongozi wa klabu kongwe ya Yanga, umekiri kuwa kipa wa timu hiyo, Beno Kakolanya anawadai fedha za usajili na si yeye pekee bali ni wachezaji wengi wanaidai klabu
hiyo, hivyo awe na subira.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa kipa huyo huenda akatimka ndani ya klabu hiyo baada ya klabu kushindwa kulipwa fedha zake za usajili kwa wakati.
Kipa huyo alijiunga na Yanga akitokea Tanzania Prisons kwa mkataba wa miaka miwili na mkataba huo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Katibu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa amesema madai ni jambo la kawaida kwa klabu yoyote, hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa na subira, kila kitu kitawekwa sawa.
"Ni kweli Beno anatudai fedha zake za usajili lakini siyo yeye peke yake, wapo wachezaji wengi ambao wanaidai klabu na wakati ukifika watapewa fedha zao, cha msingi ni kuwa na subira.
"Mimi nafahamu suala hilo na nimekuwa nikilishughulikia na kuna utaratibu wake kwa sababu wachezaji wote wangekuwa wanalalamika sasa hivi,” alisema Mkwasa.
SOURCE: CHAMPIONI
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();