IRENE WOYA ANUSURIKA KIPIGO RWANDA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 20, 2017

IRENE WOYA ANUSURIKA KIPIGO RWANDA


Staa wa bongo movie irene woya amejikuta maji shingoni pale ambapo
Mashabiki wa hayati ndikumana nchini rwanda walipo mmaind kuwa yeye amechangia tukio hilo. Wakataka kumshushia dozi lakini familia ya ndikumana ikaingilia kati na kuzuia asipigwe.
Irene aliwasili rwanda siku kadhaa akiwa na mwanae krish aliyezaa na ndikumana.
Kwa sasa staa huyo yuko kwa love na janjaro ngarenaro.

Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya.
“Mashabiki wa Ndikumana walitaka kumfanyia fujo Uwoya kwa kuwa wanadai ndiye chanzo cha kifo cha mpendwa wao, lakini familia iliwazuia wasifanye hivyo kwa kuwa walishamsamehe Uwoya ndipo hali ya amani ikawepo,” kilisema chanzo hicho. Kiliendelea kueleza kuwa, Uwoya aliwasili nchini Rwanda Ijumaa iliyopita kwenda kuona kaburi la mumewe ambaye alizikwa Jumatano iliyopita ambapo alipokelewa vizuri na mama wa Ndikumana pamoja na familia kwa jumla.
“Zile tofauti waliziweka pembeni na mama Ndikumana akamwambia wamemsamehe hivyo ikawa ni kuomboleza upya kwani Uwoya na mama’ke alikuwa akilia sana hadi kushindwa kutembea,” kilisema chanzo hicho. Hata hivyo, alisaidiwa kwa kushikwa mkono na wenyeji kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mkwewe Ndikumana kama mtoto wake.
Baada ya chanzo kutiririka, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye alikiri kupokelewa vizuri na familia pamoja na mama Ndiku ambaye alipomuona tu alimkumbatia huku akilia kwa uchungu akimuita ‘mwanangu’. Naye msanii wa filamu, Michael Sangu ‘Mike’ ambaye ni mmoja wa watu waliosafiri alikiri kuwa walipokelewa vizuri na hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza.
“Uwoya, baba, mama na Krish walitangulia na ndege na walipokelewa vizuri kabisa na hakuna mtu aliyewafanyia fujo wala nini, familia imewapokea kwa ukarimu na sisi ambao tulifika baadaye maana tulisafiri kwa basi tulipokelewa vizuri sana,” alisema Mike Sangu.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();