MABASI YAFUNGIWA KWA KUSHINDWA KULIPA KODI tsh milion 500 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 16, 2017

MABASI YAFUNGIWA KWA KUSHINDWA KULIPA KODI tsh milion 500

Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha utoaji wa huduma za usafiri kwa kampuni ya mabasi ya
Kilimanjaro Express Limited baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kampuni hiyo kutokuzaa matunda.
Kayombo amesema biashara ya mmiliki huyo kwa kipindi cha hivi karibuni haikuwa nzuri kwani mabasi yake 26 yalipungua hadi kufikia 12 lakini si kigezo cha kutokulipwa kwa kodi ya Serikali.
“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni jambo ambalo lilitufanya sisi kusimamisha shughuli tangu Jumatatu (ya Novemba 13) hadi hapo atakapolipa kodi anayodaiwa,” amesema Kayombo
Kwa upande wake, mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya amesema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro huku akieleza kuwa ni kweli anadaiwa lakini amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.
Amesema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiasi chote kilichobaki cha Sh500 milioni huku akieleza kwamba mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka na kurejea kutoa huduma
Kilimanjaro ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo Truck.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();