MAKALA: USIPOMJARI WAUBANI WAKO:ATAPEPEA KAMA PUMBA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 20, 2017

MAKALA: USIPOMJARI WAUBANI WAKO:ATAPEPEA KAMA PUMBA

Mapenzi siku zote yamegawanyika katika nyanja mbalimbali, kwenye makala haya leo, nakukumbusha wewe mwanaume ambaye umesahau majukumu yako
kama mwanaume kwa mwenza wako.
Wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kujisahau kuwahudumia wenza wao hata kwa nguo za ndani kwa kuona kuwa, kwa sababu amempata, basi hawezi kufanya hivyo.
Usijione kwa sababu umefanikiwa kumnasa mpenzi wako na sasa amekuwa mwenza wako, basi usahau majukumu ambayo awali ulikuwa ukiyafanya wakati ‘unamfukuzia’. Unaweza kudhani ni jambo dogo, lakini ukweli lina thamani kubwa sana na linaweza kukugharimu sehemu kubwa ya uhusiano wako.
Kwa mwanaume ambaye ulikuwa hujui mapenzi, huwa yananakishiwa na vitu vidogovidogo ikiwemo furaha, upendo na amani. Lakini kuna mapenzi ya dhati, uwajibikaji kwa mwanaume au mwanamke. Kitu kingine ni kujali kwa kumfanyia mambo fulanifulani mpenzi wako hasa yale ambayo anayapenda.
Kama wewe ni mwanaume ambaye umekuwa ukijijali mwenyewe kwa kujihudumia mahitaji mbalimbali kama vile kujinunulia pafyumu, boksa, nguo na vinginevyo halafu mwenza wako wala humjali.
Basi ujue wewe bado hujakamilika. Umesahau kuhusu kumhudumia mpenzi wako, unakuta mwanaume anaweza kununua nguo za zaidi ya laki moja, lakini hakumbuki kumnunulia mwenza wake japo sidiria au kufuli la shilingi elfu moja na mia tano.
Kwa mantiki hiyo, ni kama mapenzi umeyafanya yazoeleke, umemfanya mpenzi wako kama ndugu yako wa damu. Unapoacha kumhudumia mpenzi wako kwa kumnunulia nguo za ndani, unategemea nani amnunulie?
Usishangae mwenza wako akaingia kwenye mtego wa kuchepuka kwa mtu ambaye anamnunulia au kumpa zawadi hizo mara kwa mara na kumuona kama ni mwanaume ambaye anamjali.
Mwanaume aliyekamilika ni yule ambaye yupo tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kumjali, kumlinda na kumpenda mwenza wako.
Unawezaje kusimama mbele ya umati na kujiita mwanaume rijali wakati ni dhahiri huna vigezo kwa sababu huwezi hata kumnunulia mwenza wako nguo ya ndani?
Inashangaza mno kuona mwanaume ambaye yuko na mwenza wake kwa takriban miaka mitatu, lakini hajawahi eti kumnunulia angalau sidiria, hili ni tatizo ambalo wanawake wengi wamekuwa wakilalamika na kuwaona wanaume wao hawawajali.
Kama ulikuwa hujui kuhusu hilo, basi tambua kuwa kitendo cha wewe kutokumnunulia mwenza wako nguo za ndani ni kutoa fursa ya yeye kuchepuka na mwanaume ambaye ataonekana anamjali na kumpenda kwa kumnunulia vitu hivyo ambavyo wewe unavipuuza au kuviona vidogovidogo.
Wanaume wengi wanajisahau katika kuwahudumia wapenzi wao vitu vidogovidogo ambavyo kimsingi vinaweza kuwa chachu kwenye mapenzi.
Suala hili haliwahusu wanaume walio kwenye ndoa peke yao, hata wewe ambaye una mpenzi au mchumba wako. Somo hili linakufaa ili kuchachusha penzi lako. Ingawa manunuzi na mahitaji hayo unapaswa kuyafanya kutokana na kipato chako, usikubali kuvaa viatu vikubwa kuliko ukubwa wa miguu yako.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();