BODI ya mikopo yatoa awamu ya tatu na ya nne waliopata - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 13, 2017

BODI ya mikopo yatoa awamu ya tatu na ya nne waliopata

Karibu sana mainfo93 kila siku upate habari.magazeti.kudownload nyimbo mpya na season

WANAFUNZI WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WAPATA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo imetangaza orodha ya Awamu ya Nne yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia
31,353. Katika Awamu ya Kwanza , wanafunzi
10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481) na Awamu ya Tatu (7,901) .
Orodha hiyo ya Awamu ya Nne inapatikana hapa. Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi ( www.heslb.go.tz ) na imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.
Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka
2017/2018 na kati ya fedha hizo shilingi 108.8 bilioni ni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();