Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza toka Jeshi la nchi hiyo lilipoingia Ikulu juzi kwa
kile kilichoelezwa kwamba ni kutaka kumuondoa madarakani baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka 37.
Kwenye tukio lake la kwanza kuonekana hadharani toka Jeshi kuingi Ikulu juzi, Mugabe ameonekana kwenye Mahafali kwenye chuo Harare Open University huku akiwa amesindikizwa na Walinzi wake kama kawaida.
Robert Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi nyumbani kwake kwa siku mbili huku kukiwa na mvutano kuhusu nani achukue nafasi yake ya Urais ambapo hata hivyo Jeshi lilisema kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litawaambia Wananchi kuhusu matokeo ya walichozungumza.
Taarifa zinasema Rais huyo alishangiliwa baada ya kuanza kuongea kwenye Mahafali hayo ikiwa ni mara yake ya kwanza kutokea hadharani toka Jeshi lilipoingia Ikulu baada ya Mugabe kumfuta kazi Makamu wake Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita ikiashiria alikua amejipanga kumuachia nchi Mke wake