MORATA: NEYMAR ANAENDA REAL MADRID - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 12, 2017

MORATA: NEYMAR ANAENDA REAL MADRID

Nyota wa PSG, Neymar
Neymar raia wa Brazil amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid ikiwa ni miezi michache tangu alipojiunga na
PSG ya Ufaransa akitokea Barcelona ya Hispania. Nahodha wa Madrid, Sergio Ramos hivi karibuni amenukuliwa akisema milango ipo wazi kwa Neymar, 25, kujiunga nao.
Neymar ambaye aliweka rekodi ya dunia aliposajiliwa kwenda PSG kwa dau la pauni milioni 198, Agosti mwaka huu, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 11 katika mechi 12 alizocheza za michuano yote.
Morata akizungumzia tetesi hizo za usajili wa Neymar kwenda Madrid, alisema: “Ni ngumu Neymar kwenda Madrid kutokana na mambo ya huko nyuma, huyu amecheza Barcelona.
“Lakini tayari tumeona jinsi kila kitu kinavyowezekana kwa Madrid, hivyo naamini Madrid ikiamua inaweza kumsajili Neymar na kila mmoja wetu akashangaa. “Madrid wakitaka kufanya jambo, hakuna anayeweza kuzuia, hivyo kama wana nia ya kweli, basi wanaweza kumsajili Neymar.”
Madrid inataka kukiongezea nguvu kikosi chake kinachonolewa na Zinedine Zidane kwani hadi sasa kina pointi nane nyuma ya Barcelona katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ katika mechi 11
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();