JUUKO ATEMWA SIMBA - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

November 13, 2017

JUUKO ATEMWA SIMBA

     Karibu sana mainfo93 kila siku upate habari.magazeti.kudownload nyimbo mpya na season

Baadhi ya viongozi wanataka
beki huyo raia wa Uganda afungashiwe virago wakidai kuwa kwa sasa hana lolote klabuni hapo lakini wengine wanataka aendelee kubakia kwa kile walichodai kuwa bado ana mchango mkubwa katika kikosi cha timu hiyo na wengine wakihofia kusajiliwa na Yanga halafu akawatesa kama ilivyokuwa kwa Mrundi, Amissi Tambwe.
Msimu wa 2014/15, Simba ilimfungashia virago Tambwe na alipotua Yanga aligeuka kuwa mwiba mkali wa timu hiyo, jambo lilikuwa likiwaumiza vilivyo viongozi hao. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa hali hiyo imewafanya viongozi hao kushindwa kufikia muafaka wa nini kifanyike juu ya beki huyo ambaye mwanzoni mwa msimu huu ilidaiwa kuwa Klabu ya Yanga ilikuwa ikimvizia ili iweze kumsajili.
“Mabadiliko katika kikosi chetu kipindi hiki cha dirisha dogo hayatakuwa makubwa sana mpaka sasa mchezaji
ambaye anatuvuruga vichwa ni Juuko Murshid ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Desemba.
“Baadhi wanataka aondoke lakini wengine tunataka abakie kutokana na mchango wake kuwa bado unahitajika kikosini kwetu, ni kweli tuna mabeki wengi wazuri lakini baadhi yao si wazuri kama yeye, tukiachana naye katika kipindi hiki cha ushindani anaweza kutua Yanga na baadaye akaja kuwa kikwazo kikubwa kwetu kama ilivyokuwa kwa Tambwe pamoja na wachezaji wengine wengi tu.
“Hata hivyo, ngoja tusubiri tuone nini kitatokea kwani pia kabla ya kufanya maamuzi tutahitaji pia ripoti ya kocha,” kilisema chanzo hicho cha habari. Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi Kajuna hakuwa tayari kusema chochote. Juuko tangu atue Simba mwaka 2014 amekuwa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi ya timu hiyo licha ya msimu huu kukumbana na changamoto kubwa ya ushindani wa namba kutoka kwa Salim Mbonde ambaye kwa sasa ni majeruhi lakini pia kwa Mzimbabwe, Method Mwanjale.

BEKI wa kati wa Simba, Juuko Murshid, mkataba wake na klabu hiyo unamalizika mwezi Desemba, lakini hivi karibuni viongozi wa timu hiyo wametofautiana kuhusiana na mchezaji huyo.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();