Hizi ndizo nchi tajiri mwaka 2017
Tunisia ina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi na ukiachilia mbali utajiri wa mafuta na gesi, Tunisia ni nchi ambayo ina vivutio vya utalii vinavyoiingizia pesa.
9.Libya
Libya ni miongoni mwa nchi chache Afrika yenye uchumi ambao upo juu kutokana na utajiri wa gesi na gypsum zinazopatikana nchini humo na ni nchi pekee yenye utajiri mkubwa wa usambazaji wa umeme na uwekezaji wa mafuta.
8. Angola
Angola ni nchi tajiri kwa upande wa mafuta, madini ya almasi ambayo huwa yanasafirishwa kuuzwa nje ya nchi.
7. Botswana
Kiwango cha gharama za maisha kwenye taifa la Botswana kinalingana na gharama za nchi kama Mexico na Uturuki, kwa kiasi kikubwa cha uchumi wa nchi hiyo unakuzwa na uchimbaji wa madini ya Almasi na sifa yake nyingine ni kuwa na idadi ndogo sana ya watoa rushwa.
6. Gabon
Gabon utajiri wake ni kutokana na kuwa na madini na mali kwa wingi na Wafanyabiashara wengi kutoka nchi za kigeni wameweza kuifanya Gabon kuwa nchi yenye maendeleo barani Afrika kwa kuwekeza biashara zao.
5. Egypt(Misri)
Egypt/Misri ni nchi ambayo ina vivutio na hiyo inafanya kuwa na watalii wengi ndani ya nchi na nje, inatajwa kuwa ni moja pia kati ya nchi zilizostaarabika na zimeendelea upande wa kilimo,maandiko,utawala,dini,vitu vya chuma,pamba na nguo.
4. Equatorial Guinea
Equatorial Guinea ni nchi pekee Afrika inayotumia lugha ya Kispanyola kama lugha yao rasmi, wanasema moja ya vitu vinavyokuza uchumi wa nchi hiyo ni mafuta pia ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa mafuta na vingine kama kilimo, misitu na uvuvi wa samaki kwa Afrika.
3. South Africa
Uchumi wa Afrika Kusini umeimarika kwa uuzaji wa madini nje ya nchi kama madini ya dhahabu, almasi na madini mengine ya chump, hatuwezi kuisahau Afrika Kusini ilipoandaa michuano ya Kombe la dun mwaka 2010 na kuandaa kwa michuano hiyo kulichangia mapato ya nchi hiyo kuongezeka na kupata idadi kubwa ya Watalii.
2. Nigeria
Kwa mwaka 2016 IMF waliitaja Nigeria kama miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kuja kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi barani Afrika baada ya kuipiku Afrika Kusini.
1.Seychelles
Benki ya dunia mwaka 2015 ilitaja Seychelles kuwa miongoni mwa nchi zinazozoingiza mapato mengi na kukuza uchumi wa nchi hiyo, inawezekana uwepo wa idadi ndogo ya watu umesaidia nchi hiyo kuwa na uchumi imara na kufikia kuwa nchi namba moja kwa utajiri Afrika huku ikitajwa kuwa ina ukosefu wa ajira kwa kiwango cha asilimia moja pekee.