STORY:MJUKUU WA MSUKULE.
SEHEMU YA{5}.
MWANDISHI:#Amani zabranco.
Karibu sana mdau ujipatie mastery kila siku tembelea mainfo93
Sehemu iliyopita
iliishia pale mzee zagamba alipokua akihutubia mkutano wa wanakijiji kuwaabia
kua watunze hakula ili kumudu janga lililowapata, sasa endelea kutiririka
;kwa kipindi hiki cha msiba. Pia natoa
salamu za rambi rambi kwa kila aliyepoteza ndugu yake katika janga hili.
Mzee zagamba akaendelea kusema “kwa kua ,
tatizo hili ni la kwetu sote nimeamua kusimama hapa mbele yenu leo hii, ili
kutoa suruhisho la mzozo uliokua ukitusumbua kwa mda mrefu hapa kijijini.
Wanakijiji wote wakaonekana kua na hamu ya kujua jambo analotaka kusema mzee
zagamba.
Mzee zagamba
akaendelea kusema,”leo natangaza rasmi kua, mtu aliyekua akitusumbua kwa mda
mrefu, bibi kisiki cha mpingo kuanzia leo hatutaki aishi kwenye hiki kijiji,
pia kuanzia hivi sasa bibi ‘kisiki cha mpingo’ atatengwa na jamii nzima na
hakuna mtu yeyote kwenda nyumbani kwake au kuonekana akiongea nae. Kwa
atakaeenda kinyume na tamko la wakuu wa kimila atapewa adhabu ya kutengwa na
jamii kwa mda wa siku tatu ikiwa ni pamoja na faini ya ng’ombe mmoja pamoja na
gunia tatu za mpunga”.
Wanakijiji wengi wakaonekana
kushangilia huku miruzi na shangwe zikizidi kushamiri kwenye mkutano ule.
Lakini kwa pembeni kukaonekana kikundi
kidogo cha wazee wanawake pamoja
na baadhi ya kina mama vijana ambao wanaonekana kutofurahishwa na kauli ya mzee
‘zagamba’. Huku wakionekana kunong’ona chini chini.
Mzee zagamba
akahitimisha kwa kusema “sasa hivi ulinzi wa kijiji utakaa kikao ili kupanga
taratibu za kumfukuza bibi ‘kisiki cha mpingo”. Napenda kuwahimiza watu wote
mfuate niliyo tamka hapa”. Kisha mkuu wa mila akasimama ili kufunga mkutano na
kuwaamuru wana kijiji watawanyike.
Watu wakawa
wanaondoka huku minong’ono ya hapa na pale ikizidi kusikika, lakini kile kikundi
kilichokua pembeni kikawa kinaondoka kwa simanzi kuashiria kutofurahiswa na
tukio hilo.Kile kikundi kikaondoka hadi karibia na nyumba ya bibi ‘kisiki cha
mpingo’, lakini wengine wakaogopa kwenda kumsalimia wakihofia lile tamko la
kwenye mkutano. Lakini wakatokea watu watatu, wawili wakiwa ni wazee wa kike na
mmoja ni mwanamke kijana wakasema wao hawapo tayari kumtenga mtu wao wa karibu.
Wakaenda hadi kwake wale wengine
wakaendelea na safari ya kwenda makwao. Wale watatu walipokaribia kwa bibi
‘kisiki cha mpingo’ akawakaribisha huku akicheka kisha akawauliza; “vipi mbona
wengine wamepitiliza?”. Yule mmama mmoja akadakia kwa shauku “yaani kuna tatizo
kubwa,tena kubwa”. Kisiki cha mpingo akajawa na hofu akauliza……………..USIKOSE
SEHEMU YA 6 Hapahapa @mainfo93