STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART19) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

June 02, 2017

STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART19)



                                                         STORY:MJUKUU WA MSUKULE
                                                         PART(19)
                                                        MWANDISHI:Amany Zabranco
                                                        mainfo93.blogspot.com





Yule  bibi akainama chini huku chozi likimtoka kIsha akaendelea kusema ‘’nililazimishwa na mizimu ya ukoo kwa kushawishiwa na shangazi yangu lakini kila nilipokataa magonjwa yaliniandama hadi ikafikia kua kichaa, ndipo nikajikuta nimepewa huu uchawi. Ile simulizi ya yule kikongwe ikamvutia sana saguda, kIsha yule bibi akaendelea kumpa saguda mbinu za kutoroka pale gamboshi,lakini akamuambia kuwa si kazi rahisi kuweza kutoroka kwenye ile himaya ya wachawi kwa kuwa kila kona kuna ulinzi wa mizimu.
Yule bibi akasema kuwa atamlinda ili asikatwe ulimi kama ndondocha wengine, mara
wakaja walinzi wakasema ‘’tunamhitji huyo aende akale na misukule wenzake, yule bibi akawajibu kuwa ‘’mimi nitampa chakula huyu,nitampa mimi mwenyewe’’. Wale walinzi wakasema kuwa  ‘’masharti ni lazima akale na misukule wenzake’’. Wakamchukua saguda kwa nguvu, yule  bibi akawaambia kuwa akimaliza kula wamrudishe kwake.

Saguda alipofika  chumba cha misukule  akawa anaogopa kusogeleana na misukule kwa kuwa walikua wanatisha , saguda akajibana kwenye pembe ya kona ndani ya kile chumba. Baada ya muda mfupi chakula kikaletwa kisha walinzi wakakitenga katikati ya misukule huku wakikisukuma kwa miguu, ghafra misukule wote wakalisogelea  lile sufuria  wakaliinamia na kuanza kukigombania kile chakula.
Saguda akabaki anawashangaa huku akiwa amejibana kwenye pembe ya kile chumba  kwa kua hata hamu ya kula hakuwa nayo kabisa kwa jinsi wale misukule walivyokuwa wanatisha. Walipomaliza kugombania kile chakula, saguda akamuona msukule mmoja akagundua kuwa ni bibi yake aliye kufa miaka mingi iliyopita. Saguda akabaki na maswali mengi kichwani akawa anawaza. Mara yule bibi ambaye ni msukule akakumbuka kuwa saguda ni mjukuu wake, akamsogelea akaanza kumuangalia usoni.

Saguda akawa anamuogopa japokuwa ni bibi yake. Yule bibi akawa najaribu kumuita saguda lakini sauti ikawa haitoki kwa kuwa alikuwa kishakatwa ulimi , Sagauda akawa anakumbuka kuwa aliambiwa na yule kikongwe kuwa jina lake litakuwa ni ‘mjukuu wa msukule’ kwa kuwa lina nyota ya kupambamna na wachawi. Wakati saguda anaendelea kumuangalia yule  bibi, mara msukule mwingine akamsogelea  saguda. Kisha yule msukule akamuangalia yule bibi wakawa wanaongea kama mabubu  lakini wao wakawa wanaelewana, saguda akawa anamuogopa yule msukule huku mapigo ya moyo yakimdunda kwa kasi, yule msukule akagundua kuwa kumbe saguda alikuwa ni mjukuu wa yule bibi msukule. Kisha yule msukule akamsogelea saguda , msukule akajichoma kwenye kidole  damu ikaanza kutoka akawa anaitumia ile damu kuandika chini ili saguda aelewe.

Msukule akaandika ‘’ usiniogope mimi ni mtu mwema, huyu hapo ni bibi yako, kwa hiyo wewe ni mjukuu wa msukule’’. Hapo saguda akawa na Amani kidogo, wakaanza kuwasiliana na yule msukule kwa kuandikiana maneno pale chini. Yule msukule akamuomba saguda wawe marafiki saguda akakubali  . Mara akaingia yule kikongwe akiwa na wale walinzi aka………………….(ITAENDELEA)
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();