STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART(20)
MWANDISHI:Amani Zabranco
Mara
akaingia yule kikongwe akiwa na wale walinzi, akasema anataka kuondoka na
Saguda, Saguda akamuomba yule kikongwe kua atoke pamoja na yule rafiki yake
aliyempata mule ndani ya chumba cha misukule. Yule bibi akamkubalia na wote
wawili wakatoka kuelekea kwenye jengo la Yule kikongwe.
Walipofika mule ndani yule
kikongwe akamuuliza Saguda kama amekula, lakini Saguda akajibu kuwa hajala
chochote, Yule bibi akamletea chakula
kizuri cha kawaida kisha Saguda akala hadi akatosheka.
kizuri cha kawaida kisha Saguda akala hadi akatosheka.
Miezi nane ikapita huku
kila mbinu aliyokuwa anaipanga Saguda kwa ajiri ya kutoroka ikawa
inashindikana, siku moja yule bibi akawaita saguda na rafiki yake yaani yule
msukule aliyejuana naye pale gamboshi. Kisha kikongwe akawapa ramani nzima ya
kutoroka pale gamboshi. Akawaambia kwamba, ‘’kwanza inabidi mkatafute kibuyu
ambacho kipo kwenye pango kubwa ambalo lipo ndani ya h ii himaya, hicho kibuyu
ndiyo kina dawa ambayo mtu akijipaka wachawi wala mizimu haiwezi kumuona’’.
Yule bibi akaendelea
kuwapa ramani nzima, akawa anawaambia kuwa ndani ya pango ambapo ndipo kuna
hivyo vibuyu, kuna nyoka mkubwa wa ajabu na mkali ambaye anavilinda hivyo
vibuyu. Saguda aliposikia vile akaanza kuwaza jinsi kazi ya kutoroka
itakavyokuwa ngumu, yule rafiki yake na Saguda akakubali hata kufa ili Saguda
afanikishe kuipata ile dawa.
Kikongwe akatoa hirizi
nyeusi akampa Saguda akamuambia kuwa itawasaidia ili mizimu isiwadhuru
wanapoingia kwenye lile pango. Lakini yule kikongwe akawaambia kuwa wakikamatwa
wasimtaje kwa kua ataonekana ni msaliti ndani ya ile himaya.
Mara Sauti za ngoma
zikasikika kwa nje, yule bibi akasema ‘’leo ni siku ya kula nyama ya mtu kuna
watu wa kutolewa kafara wameletwa, kwa hiyo gamboshi nzima inasherekea kwa kula
nyama zao!!!’’. Saguda naye akawa na hofu kuwa huenda akala nyama ya mtu,
saguda akaamua kumuuliza yule bibi ‘’bibi hivi hata mimi watanilazimisha kula
nyama ya binadamu????’’. Yule kikongwe akasema kuwa sheria ni lazima watu wote
pale gamboshi washiriki kwenye hiyo sherehe ikiwa ni pamoja na kula nyama za
watu.Firimbi na ngoma zikazidi kutawala kwa kule nje, yule bibi akamuambia
saguda kuwa inabidi waende chini ya mti wa mbuyu ambapo ndipo ngoma zinapigwa,
lakini kikongwe akamuambia yule rafiki yake na saguda aondoke na arudi kwenye
kile chumba cha misukule, kwa kuwa misukule hawaruhusiwi kujichanganya na watu
wengine.
Yule bibi akasema inabidi kwanza ampeleke saguda
jikoni ili akaone mapishi ya gamboshi jinsi yalivyo. Wakaondoka na Saguda
kuelekea jikoni kwa kuwa yule bibi alikuwa ni mkuu wa kitengo cha mapishi pale
gamboshi, walipofika jikoni Saguda hakuamini macho yake kuona masufuria makubwa
yakiwa yamejaa vipande vya nyama za watu. Saguda akazidi ku……………….(USIKOE
SEHEMU INAYOFUATA @ mainfo93.blogspot.com)